Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imesema inajivunia kuwa sehemu ya mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika –SADC na kutoa huduma bora za mawasiliano kwa wajumbe wanaoshiriki Mkutano huo.

Ushiriki wa Airtel katika Mkutano huo ni pamoja na kutoa line za simu za mtandao huo Bure, kutoa huduma ya Airtel Money yaani kutuma na kupokea pesa kwa wajumbe ambao wanatoka katika nchi ambazo Airtel inatoa huduma na pia wanatoa huduma kwa wateja wakubwa ambao wanahudhuria Mkutano wa SADC.

Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano amesema, kuwa watumiaji wa Mtandao wa Airtel kutoka katika nchi za Zambia, Shelisheli, Malawi, Madagascar pamoja na Tanzania ambao ni wenyeji wanaendelea kufurahia huduma za mawasiliano kupitia mpango wa One Network.

Bi Singano amesema kuwa wameamua kutoa laini za Airtel bure kwa wajumbe wa SADC ili waweze kufurahia huduma za mawasiliano wakiwa hapa nchini na pia kuwawezesha kufurahia huduma nyingine.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kitengo cha wateja wakubwa wa Airtel Alice Mashiku amesema, kampuni hiyo inashiriki Mkutano wa SADC ili kuwahudumia wateja wao wakubwa kutoka katika nchi za Zambia, Malawi, Shelisheli na Madagascar na pia kutoa huduma mbalimbali kwa wajumbe wengine wa Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...