Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (aliyevaa shati jeupe) akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mh. Tae-ick-Cho ambaye leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
Balozi Tae-ick-Cho akizungumza jambo wakati wa kikao hicho mapema hii leo katika Hospitali ya Mloganzila.
Baadhi ya viongozi wa MNH-Mloganzila pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Korea nchini , wakimsikiliza kwa makini Balozi Tae-ick-Cho ambaye ameahidi kushirikiana na Hospitali ya Mloganzila katika kutatua changamoto zilizopo.
Balozi Tae-ick-Cho (wa kwanza kulia) akiwa na ujumbe wake, wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumalizika kwa kikao, wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
Balozi Tae-ick-Cho (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru (kushoto), kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.

Na Neema Wilson Mwangomo

Balozi wa Jamhuri ya Korea Tae-ick-Cho leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kuahidi ushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Pamoja na mambo mengine katika mazungumzo hayo, Balozi Tae-ick-Cho pia amezungumzia jinsi ya kuboresha mfumo wa TEHAMA uliokuwepo katika kusimamia utoaji wa huduma za afya hospitalini.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema watanzania wanapenda kuona hospitali hii ikifanya kazi iliyokusudiwa ya kutoa huduma, elimu na utafiti na kusisitiza kuwa hilo ndio kusudio kubwa la Rais John Magufuli.

“Lengo letu ni kuhakikisha hospitali hii inafanya kazi kama inavyotakiwa hasa ukizingatia ni hospitali kubwa na ya kisasa hivyo tutaendelea kuboresha huduma zetu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa” amesema Prof. Museru.Balozi Tae-ick- Cho mapema hii leo amefika MNH-Mloganzila kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na uongozi wa hospitali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...