Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

BARAZA la Ardhi na Nyumba wilaya ya Arusha limetengua umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa hekari 15 iliyokuwa ikimiliwa na mwanajeshi mstaafu,Willison Rugumam aliyejenga kituo cha watoto yatima cha Huruma Vision Tanzania na kulirejesha kwa wananchi wa kata ya Sokoni one katika Jiji la Arusha.

Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita ,katika kesi ya Ardhi Namba 147 ya mwaka 2012 iliyofunguliwa na Rugumam akiwalalamikia wananchi saba wa kata ya Sokon I kwa kuvamia eneo hilo na kufanya uharibifu ,mwenyekiti wa baraza hulo,Fadhili Mdachi alidai kuwa mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha uhalili wa yeye kuwa mmiliki wa eneo hilo hivyo baraza limetupa maombi yake.

Mdachi amesema kuwa Rugumam alipeleka maombi ya kutaka baraza hilo limtambue yeye kama mmiliki halali wa eneo hilo lakini ushahidi alioutoa kupitia mashahidi wake saba umekosa mashiko ya kulishawishi baraza hilo limtambue kama mmiliki halali wa eneo hilo.

Katika hukumu hiyo ,Mdachi alizingatia kuwa mlalamikaji hakuwa amekabidhiwa eneo hilo kihalali kupitia mkutano mkuu wa Kijiji cha Sokoni I,na kwamba hapakuwa na makubaliano yoyote kwamba àtajenga ofisi ya Kijiji kama mbadala wa eneo hilo badala yake baraza hilo limeonelea kuwa afisi ya Kijiji aliyojenga ,alifanyahivyo kama mfadhili na si makubaliano ya kupatiwa eneo kama alivyodai.

"Baraza limepitia ushahidi wa pande zote mbili na kuonelea kwamba ushahidi wa upande wa utetezi unauzito kwani ugawaji wa eneo hilo haukupata baraka za mkutano mkuu wa Kijiji na kwamba halmashauri iliyomgawia eneo hilo haikuwa na muhtasari wa mkutano mkuu uliokubaliana eneo hilo ligawiwe kwa malalamikaji" Alisema Mdachi

Mwenyekiti wa baraza hilo amelirejesha eneo hilo kwa wananchi baada ya kuwatambua kama wamiliki halali wa eneo hilo na kumtaka Rugumam kukata rufaa ndani ya siku 45 iwapo kama hajaridhika na maamuzi hayo.

Nje ya mahakama baadhi ya wananchi waliokuwa wamefurika kusikiliza shauri hilo lililodumi kwa takribani miaka saba walilipuka kwa shangwe na kulishukuru baraza hiyo na kudai kwamba haki imetendeka na watalitumia eneo kwa shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha Polisi ,shule na zahanati .

Shauri hilo lilifunguliwa katika baraza hilo , mwaka 2012 na mlalamikaji Wilson Rugumam akiwalalamikia wananchi saba wa kata ya sokono I kwa kuhamasisha wenzao waliokuwa kwenye mkutano kuvamia na kufanya uharibifu wa mali na ukuta wakati wanajua kwamba eneo hilo ni mali yake.

Kufuatia hukumu hiyo Rugumam aliyekuwa ameambatana na mkewe katika baraza hilo alishindwa kufafanua iwapo anajipanga kukata rufaa au ameridhika na hukumu hiyo badala yake alidai kuwa anaenda kutafakari na familia yake juu ya nini cha kufanya.
Picha ikionyesha Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Muriet Kata ya Sokoni 1,Wakishangilia ushindi katika baraza la Ardhi na Nyumba Arusha Mara baada ya kurejeshewa Ardhi yao yenye ukubwa wa ekari 15 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...