Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi Abdalla Ulega amesema kuwa Elimu na ujuzi Wa vitendo ipelekwe kwa wakulima wa vijijini pamoja na wafugaji ili kuwa na wafugaji wenye kufuga kisasa na hatimaye kuchangia katika kufikia uchumi Wa viwanda kama kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu ya nane nane inavyosema Kilimo ,mifugo na uvuvi kwa ukuaji Wa uchumi Wa nchi.

Ulega ameyasema hayo Leo wakati akifunga maonesho ya 26 ya kilimo na mifugo (nanenane )kwa Kanda ya kaskazini yalikuwa yakifanyika katika viwanja vya Themi Njiro ambapo alisema kuwa kwakuzingatia kauli mbiu maarifa haya yaliotolewa katika maonyesho haya yasipoishia hapa nchi yetu itajitosheleza kwa chakula na mifugo na hatutakuwa na haja ya kuitaji chakula cha msaada bali tutakuwa na chakula cha kutosha .

Alibainisha kuwa tukichukuwa ujuzi huu tulioupa hapa tutapata mazao bora na mifugo ambapo tutauza mazao ya kilimo na mifugo kibiashara ndani ya nchi na nje ya nchi pia tutaacha kuwa wazalishaji Wa malighafi kwa nchi zingine pia tutaacha kuhamasisha Elimu za viwandani kwenda nchi zingine endapo tutawekeza katika viwanda badala yake tutavuta wawekeza kutoka nchi zingine na kuja kuwekeza katika viwanda ndani ya mikoa hii ya Kanda ya kaskazini ambapo watakuwa na uhakika Wa kupata malighafi bora za Kilimo mifugo na uvuvi

Aidha alitoa wito kwa wakuu Wa mikoa ya Kanda ya kaskazini ,Wakuu Wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanatoa huduma staiki kwa maofisa ugani ili waweze kuwahudumia vyema wakulima na kuwajengea uwezo waweze kufikia dhamira ya kuongeza uzalishaji ,kuongeza dhamani,pamoja na kipato katika familia na hatimaye kuuza kibiashara .

"Napenda kuwasisitizia wakuu Wa mikoa kuwasimamia vyema wakurugenzi Wa halmashauri na wakurugenzi Wa halmashauri kusimamia vyema wakulima kulima Kilimo chenye tija pamoja na wafugaji ili kuleta chachu ya maendeleo ili wanapo uza bidhaa zao waweze kuongeza pato lao na pato la Taifa kwa ujumla "alisema Ulega

Alisema kuwa maafisa ugani wamekuwa Wanatumika zaidi kuonyesha uwezo wao Wa nadharia zaidi katika viwanja vya maonyesho badala ya kuonyesha ujuzi wao Wanadhari kwa wakulima Wa vijijini .

Kwa upande wake Mkuu wa mikoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye mi mwenyeki wa maonyesho haya alisema kuwa mwitikio kwa mwaka huu umekuwa mkubwa hususa ni kwa wafugaji tofauti na miaka ya nyuma na hata ongezeko la uongezwaji thamani mazao ya mifugo umeongezeka .
   Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi  Abdalla Ulega akihutubia wananchi wakati akifunga sherehe za maonyesho ya nanenane  Kanda ya kaskazini yaliofanyika jijini Arusha
 bendi ya Polisi Moshi ikitumbuiza mbele ya mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini yaliyofanyika njiro Themi jijini hapa.
 Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi  Abdalla Ulega akimkabidhi kombe la ushindi mkurugenzi wa TAHA Jacqueline Mkindi Mara baada ya kushinda katika sherehe za wakulima Kanda ya kaskazini.
Mkuu wa chuo cha Uhasibu Njiro,Prof.Eliamani Sedoyeka  kulia akipokea zawadi ya kombe kutoka kwa Naibu Waziri Mh. Ulega

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...