Chama cha Wataalam wa Magonjwa ya Dharura na Tiba Tanzania (EMAT) kimetoa mafunzo kwa wataalam wa magonjwa hayo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalam wa magonjwa ya dharura wa hospitali hiyo ili waweze kutoa huduma za magonjwa ya dharura na kuepusha vifo vinavyosababishwa na kukosekana kwa huduma hiyo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dkt. Kilalo Mjema amesema mafunzo hayo yaliendeshwa kwa siku nne na yametolewa kwa wataalam wa idara tofauti katika hospitali hiyo.

“Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha watoa huduma kuweza kukabiliana na magonjwa ya dharura na kuzuia vifo vinavyoepukika kwa kupatiwa huduma hiyo, pia ni muhimu kila mtu kufahamu hatua za awali za kusaidia mgonjwa wa dharura,” amesema Dkt. Kilalo Mjema.

Dkt. Kilalo amesema kwamba katika mafunzo hayo watoa huduma wamejengewa uwezo wa kumsadia mgonjwa ambaye amepata mshtuko wa moyo (Cardiac Arrest)

Katika mafunzo hayo, watoa huduma wameshauriwa kuwa na uharaka wa kutambua mgonjwa na aina ipi ya uhuduma ya awali apatiwe kuokoa maisha yake, pia wamejengewa uwezo wa kushirikiana katika utoaji wa huduma kiufasaha
Dkt. Adyson Mpyambala akifanya mafunzo kwa vitendo namna ya kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo la kupua kwa kutumia kifaa maalumu cha kusaidia upumuaji kwa lugha ya kitaalamu bag valve mask ventilation.
 Wataalam wa magonjwa ya dharura wakimsikiliza Dkt. Kilalo Mjema wakati akifundisha mbinu mbalimbali ambazo wanapaswa kuzitumia kuokoa maisha ya wagonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...