Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BARAZA la Kamati ya  Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)  leo Agosti14  wamekubaliana na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya jumuiya hiyo huku wakieleza kuwa kwa sasa wanasubiri baraka za wakuu wa nchi hizo ili ianze kutumika.

Akizungumza mara baada ya kikao cha mawaziri wa SADC , Mwenyekiti wa kamati ya baraza hilo la mawaziri wa SADC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na uUhirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema baada ya baraza la mawaziri kukaa kwa siku mbili wametoka na mapendekezo 107 ambayo yatapelekwa kwa wakuu wa nchi kwa ajili ya majadiliano yatakayofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

"Mkutano wa mawaziri hautoi maamuzi bali uamuzi utatolewa na wakuu wa nchi baada ya kukaa katika kikao cha siku mbili, moja ya pendekezo kubwa na lenye kuleta heshima kwa watanzania ni kuichagua lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ambayo itatumika katika ngazi mbalimbali ikiwemo katika vikao vya baraza la mawaziri, vikao vya wakuu wa nchi, hotuba mbalimbali na baadaye kutafsiriwa katika nyaraka mbalimbali" ameeleza Kabudi.

Pia amesema katika mapendekezo hayo ambayo yamejikita katika kauli mbiu ya mazingira wezeshi ya biashara na ukuaji wa viwanda ndani ya jumuiya wanachama kwa muda wa mwaka mmoja uenyekiti utakaoongozwa na Rais. Dkt. JohnJoseph Magufuli utahakikisha biashara inakua katika ukanda wa SADC.

"Tupo chini sana katika masuala ya umiliki wa biashara tunamiliki asilimia20 pekee huku asilimia 80 tukizitumia kununua bidhaa kutoka nje hali inayokosesha ajira kwa vijana wetu" ameeleza.

Aidha amesema kuwa kwa muda wa mwaka mmoja wa uenyekiti Tanzania itahakikisha  asilimia 60 ya vijana ambalo ndilo kundi kubwa linapata ajira aidha kwa kujiajiri au kuajiriwa na hiyo ni kwa kuhakikisha biashara zinafanywa kwa kuhusisha nchi zote wanachama na pia watahakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha Zimbabwe inaindolewa vikwazo walivyowekewa na baadhi ya nchi na hiyo ni baada ya nchi hiyo kufanya uchaguzi na kubadilisha mifumo mbalimbali hivyo hakuna sababu ya kuwekewa vikwazo ambavyo huwaumiza wananchi.

Mapendekezo hayo 107 yatajadiliwa na kufanyiwa maamuzi katika kikao Cha wakuu wa nchi na Serikali kitakachofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akigonga meza kuashiria kufungwa kwa kikao cha kamati ya baraza hilo kilichokutana kwa siku mbili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dkt Stergomena Tax .
Washiriki wa kikao cha Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC)wakiwa wamesimama wakati wimbo wa jumuiya hiyo na wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa ukumbini hapo leo Agosti 14, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi JR
Washiriki wa kikao cha Kamati ya Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC wakiwa wamesimaam wakati wimbo wa jumuiya hiyo ukiendelea kabla ya kufungwa kwa kikao cha kamati hiyo kilichoketi leo Agosti 14,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam 
Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC wakifuatilia kikao katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo 
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) Profesa Palamagamba Kabudi akizunguza leo Agosti 14,2019 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa akifunga kikao cha baraza la mawaziri hao ambacho kimekutana kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo 
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) Profesa Palamagamba Kabudi akizunguza leo Agosti 14,2019 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa akifunga kikao cha baraza la mawaziri hao ambacho kimekutana kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo.Picha na Michuzi JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...