Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Alhaji Sibatin Meghjee (kulia) akimkabidhi hati ya kamabidhiano ya vyoo nane kati ya 20, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) jana.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kulia) akifungua mlango wa moja ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Nyuma ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) akifungua bomba na kwenye sinki la maji nje ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) akifungua bomba na kwenye sinki la maji nje ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.

************
NA BALTAZAR MASHAKA

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure imemtunuku na kumkabidhi cheti Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Cair Foundation (TD &CF), Alhaji Sibtain Meghjee kwa a kutambua mchango wake wa kusaidia jamii.

Alhaji Meghjee alikabidhiwa cheti hicho jana na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Bahati Msaki muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi matundu nane ya vyoo kwenye hospitali hiyo yaliyotolewa na The Desk & Chair Foundation na kugharimu sh. zaidi ya sh. milioni 20.3.
Akimkabidhi cheti hicho Dk Bahati alisema, Alhaji Meghjee kupitia taasisi hiyo amejitoa na kufanya mambo mengi kwenye jamii na kujenga miundombinu ya jengo la kupumzikia pamoja na vyoo matundu saba kwa ajili wananchi wanaokuja kuona wagonjwa kwenye hospitali hiyo.

Pia amejenga vyoo matundu manne kwenye jengo la kuhifadhia maiti ikiwa ni pamoja na kutoa msaada waa manteki ya kuhifadhia maji, madawa na vifaa tiba pamoja na mgodoro kwa ajili ya wagonjwa.

“Tutakuwa ni wezi wa wafadhila tusipoenzi na kutambua mchango wa Alhaji Meghjee na taasisi yake katika kusaidia jamii ikiwemo hospitali hii na wapokea huduma wake.Hivyo tunamkabidhi cheti hiki ikiwa ni kumbukumbu yake kwa mazuri aliyotufanyia hospitali ya Sekou Toure,”alisema Dk.

Kwa upande wa alhaji Meghjee alishukuru kwa cheti hicho na kuahidi kitakuwa chachu ya kuendelea kusaidia jamii.

“Najisikia faraja kwa kupata zawadi hii ambayo itakuwa chachu ya kuendelea kusaidia jamii katika sekta mbalimbali kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wananchi wanatimiza ndoto zao,”alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...