Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya uchunguzi katika Wilaya ya Bumbuli ambapo Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo alisimamishwa.

Mhe Jafo ameyasema hayo katika Kikao kazi cha Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma ambapo kinalenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa Afya wa mwaka uliopita.

Amesema Wizara ya TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itahakikisha kuwa pamoja na Uwekezaji mkubwa inaoufanya katika Sekta hiyo ni lazima wahakikishe pia wanawalinda watumishi wake.

" Mimi Niwapongeze sana ndugu zangu madaktari mnafanya kazi kubwa sana katika kuwatumikia wananchi wetu, kama Wizara hatutokubali kuona mtu yeyote anawagandamiza, nyinyi ni nguza kubwa na mnastahili sifa na heshima kwa utumishi wetu.

" Ni kweli tumejenga vituo vingi vya Afya na Hospitali Nchi nzima vilivyogharimu Bilioni 385. Lakini pia ni jukumu letu kuwajengea watumishi wetu mazingira rafiki ya kufanya kazi zao kwa weledi, niwaahidi lazima tuwalinde," amesema Waziri Jafo.

Aidha amemuagiza Katibu Mkuu pia kuhakikisha watumishi saba wa Kituo cha Afya Ipogoro kilichopo Manispaa ya Iringa waliokua wameondolewa kazini kurudishwa mara moja na tayari ameshaunda Timu inayofanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha watumishi hao kuondolewa katika Kituo chao cha kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amewataka madaktari kuongeza ubunifu na kujituma zaidi katika vituo vya vya kazi.

Amesema wao kama wataalamu wana jukumu la kuhakikisha wanazuia Watanzania kutokuugua na kuwataka kuwa suluhishi na siyo walalamikaji.

" Madaktari tunapaswa kuongeza ubunifu, mfano juzi kuna mmoja kanipigia simu ananiambia Hospitali yake haina Thermometer sasa kama kifaa kidogo hicho anashindwa kununua mpaka Serikali Kuu ije kuna maana gani ya yeye kuwa kwenye nafasi hiyo? Kwani Hospitali haina mapato?.

" Ni lazima tubadilike, na ninafikiri ni vema mkutano ujao tuitaje Mikoa iliyofanya vizuri na kuipa zawadi lakini pia ile iliyofanya vibaya nayo itajwe," Amesema Dk Ndugulile.

Nae Rais wa Chama Cha Madaktari Nchini ameipongeza Serikali chini ya Rais Dk John Magufuli kwa namna ilivyoboresha vituo vya Afya jambo ambalo linawafanya sasa wao ndio wawe na deni kwa Mhe Rais LA kutoa huduma bora kwa wananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...