Na Lusako Mwang’onda, Mahakama Kuu – Iringa 

Jumla ya mashauri 29 yanatarajiwa kusikilizwa mkoani Iringa katika kikao maalum ‘session’ ya Mahakama ya Rufani chini ya jopo la Wahe. Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma. 

Akizungumzia kuhusu kikao hicho ‘session’ mapema Agosti 19, 2019, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eddie Fussi amesema kuwa katika kikao hicho kuna jumla ya mashauri ya rufaa za jinai ishirini na tano (25), rufaa za madai mbili (2) na maombi ya madai mawili (2) 

Mhe. Fussi ameongeza kuwa kati ya mashauri hayo ishirini na tisa (29); matatu (3) ni ya zamani (backlogs) na ishirini na sita (26) ni ya muda wa kati na mapya (back stopping). 

Kikao hiki cha Mahakama ya Rufani kilichoanza wiki iliyopita ni cha pili (II) kufanyika ndani ya mwaka huu. Majaji wengine waliopo katika jopo hilo ni pamoja na Mhe. Richard Mziray, Mhe. Rehema Mkuye na Mhe. Ignas Kitusi. 

Kikao hicho kitarajiwa kukamilika Agosti 30 mwaka huu na mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho, Mhe. Jaji Mkuu anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwenye Mahakama zote za mikoa ya Iringa na Njombe, ambapo atakagua maendeleo ya shughuli mbalimbali za kimahakama na kuzungumza na watumishi. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni Agosti 18, 2019 pindi alipowasili mkoani Iringa kuungana na jopo la Majaji watatu katika kikao maalum cha Mahakama ya Rufani ‘session’ kinachofanyika mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...