Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzichukulia hatua kampuni zote za mawasiliano nchini ambazo hazijatekeleza agizo la serikali la kuhakikisha gharama za kupiga simu kwa dakika kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine inakuwa Sh. 10 na Senti 40.

Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia sekta ya uchukuzi na mawasiliano, Atashasta Nditiye wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kutoka Zanzibar Dk. Sira Mamboya. 

Alisema kuwa amekuwa akisikia matangazo ya kampuni mbalimbali za simu katika redio na televisheni ambayo yanasema kuwa kupiga simu ni Shilingi moja kwa sekunde jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Serikali.

Nditiye amesema TCRA inapaswa kulifatilia suala hilo kwani gharama zilizowekwa na Serikali ni Shilingi 10 na Senti 40 kwa dakika kufanya Shilingi moja kwa sekunde ni sawa na Sh. 60 kwa dakika. 

"Mwishoni mwa mwaka jana niliutangazia umma wa Watanzania kuwa kuanzia Januari Mosi mwaka huu zile gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine itakuwa ni Sh. 10 na Senti 40 lakini jambo hili wala halijatekelezeka mpaka sasa na kampuni za simu, kwahiyo nawataka TCRA wafatilie kampuni zote ambazo hazijatekeleza utaratibu huu maana vifaa vyote wanavyo," alisema na kuongeza 

"Mawaasiliano ni haki ya kimsingi ya kila mtu na tunahitaji wananchi waweze kumudu gharama za kupiga simu, natambua kuwa teknolojia hii inakua kila siku na watu ubuni vitu vipya ikiwamo wizi na ujanja ujanja ambao kiukweli TCRA wanapambana nao, ila katika suala hili la gharama kampuni hizi alijazitekeleza hivyo ni wajibu wa TCRA kulifuatilia na kuwachukulia hatua, " alisema. 

Aidha Waziri Nditiye amewataka wananchi wote nchini wanaomiliki simu za mkononi kuendelea kusajili laini zao kwa alama ya vidole. Mbali na hayo, Waziri Nditiye alisema katika wizara hiyo sekta ya mawasiliano ni ya muungano hivyo amejisikia faraja kwa waziri wa Zanzibar kuja kutembelea mamlaka hiyo kwa lengo la kujifunza vitu mbalimbali. 

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya amesema TCRA ni chombo cha muungano hivyo yeye kama Waziri ameamua kuja kujifunza na kuangalia jinsi kinavyofanya kazi. 
Amesema kila baada ya muda vikao vya baraza la wawakilishi ufanyika na kunakuwepo na maswali kuhusu TCRA hivyo kuja kwake anaamini atajifunza mengi yatakayomsaidia kuweza kujibu maswali hayo.
Naibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana uendeshaji wa mamlaka hiyo wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia uendeshaji wa mawasiliano nchini katika Ofisi za Makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Connie Francis akizungumza kuhusiana na utendaji wa TCRA Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya na watendaji wake walipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Victor Kweka namna wanavyoangalia masafa katika gari maalum wakati waziri huyo alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa akipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa Makumbusho ya TCRA Jasmine Kiyungi wakati waziri huyo alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...