Na Editha Karlo Michuzi tv,Kigoma

SEREKALI ya Tanzania kupitia uratibu wa wa ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto zitafanya zoezi la kupima utayari wa sekta ya afya,wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola endapo utatokea.

Bashiru Taratibu mkurugenzi msaidizi wa utafiti na mipango idara ya menejimenti maafa ofisi ya Waziri Mkuu aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha wadau mbalimbali watakaoshiriki katika zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na mazoezi ya utayari.

Alisema kuwa zoezi hilo litazingatia dhana ya afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya mifugo,binadamu,mifugo,wanyamapori na mazingira katika kujiandaa,kufuatilia na kukabili magonjwa ambayo huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda binaadam."Zoezi hili litapima uelewa wa jamii kuhusu namna ambavyo wanapaswa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola ukitoke hivyo wakati wa zoezi watoa huduma za afya na sekta zingine watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo"alisema

Alisema zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Agosti katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya mipaka ya Mkoa wa Kigoma.Taratibu alisema kuwa katika zoezi hilo watoa huduma wa afya watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo namna ha kumuhudumia mgonjwa wa ebola atakapogundulika.

Mgeni rasmi katika kikao hicho Daniel Machunda katibu Tawala msaidizi rasilimali watu kwaniaba ya katibu wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchata alisema Mkoa wa Kigoma una njia nyingi zisizo za halali za mipakani(panya road)ambazo zinachangia hatari ya ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa wale wanaovuka mipaka kwenda nchi za jirani."Ikumbukwe kuwa zoezi nila kupima utayari utayari kwa Mkoa wa Kigoma na hakuna mgonjwa yeyote wa ebola aliyeripotiwa hadi sasa nchini"alisema Machunda

Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alisema kuwa nchi ya jirani ya DRC(Congo)imeendelea kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti 2018 hadi tarehe 31 Julai 2019 jumla ya watu 2673 waliathiriwa na ugonjwa huo.

Alisema idadi ya vifo vilikuwa 1823 ikiwa ni sawa na asilimia 67 ya idadi watu walioathiriwa na ugonjwa huo huku nchi ya Uganda ambayo inapakana na DRC na Tanzania imekuwa na wagonjwa 3 wa Ebola kwa mujibu wa taarifa maambukizi hayo yametoka DRC.

"Kwenye mipaka yetu ya DRC na Burundi kuna mwingiliano mkubwa wa watu unaochangiwa na shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi hivyo vinachangia hatari zaidi ya ugonjwa wa Ebol kuingia nchini"alisema Dkt Chawote

Remidius Kakulu Afida Afya mwandamizi toka Wizara ya afya,jinsia,wazee na watoto alisema kuwa mpaka sasa mipaka iliyorasmi yote imethibitiwa na serikali imeshafunga vipima joto vya kisasa katika mipaka yote iliyo rasmi.

"Kuna ile mipaka ambayo siyo rasmi ambayo ipo kwenye vijiji na maeneo mengine tunawaomba viongozi wa vijiji pamoja na wananchi kutoa taarifa pale mgeni anapoingia au kumpeleka kituo cha afya ili aweze kupimwa"alisema
 Mgeni rasmi Daniel Machunda katibu msaidizi rasilimali watu akifungua kikao cha washiriki wa zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola
 Baadhi ya washiriki wa zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola wakimsikiliza mtaalam toka Wizara ya afya.
 Viongozi wa meza kuu kutoka Shirika la afya Duniani,Wizara ya afya,jinsia,maendeleo wazee na watoto pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa juu ya zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola
Washiriki kutoka halmashauri nne za Mkoa wa Kigoma wa zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola wakiwa katika picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...