Shirika la reli Tanzania - TRC lapokea Ugeni wa mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC ambao wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.

Ugeni huo mkubwa ulipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa katika eneo ambalo stesheni kubwa ya reli ya kisasa inajengwa Stesheni jijini Dar es Salaam na kuwapa maelezo kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa - SGR ambao ulianza mwaka 2017 chini ya Mkandarasi Yapi Merkezi ambapo mradi unatekelezwa kwa kusanifu na kujenga.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja kungu Kadogosa alielezea faida za Mradi ikiwemo ajira zilizozalishwa kupitia mradi ambapo 96% ya wafanyakazi katika mradi huo ni Watanzania, pia Mkurugenzi ameeleza kuwa shirika linaendelea na mpango wa kuandaa vijana watakaosimamia na kuendesha shughuli za usafirishaji katika reli ya kisasa ambapo vijana wanapewa mafunzo ya nadharia na vitendo nje na ndani ya nchi ili mradi utakapokamilika kuwe na nguvu kazi ya kuweza kuendeleza mradi huo mkubwa.

“Katika miradi mikubwa inayosimamiwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mh. Rais Dr.John Pombe Magufuli Ujenzi wa Reli ya Kisasa ni mmoja wapo” alisema Ndugu Kadogosa.

Vivyo hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TRC alitolea ufafanuzi juu ya tofauti zilizopo kati ya Reli ya kisasa - SGR inayojengwa Tanzania na za nchi nyingine barani Afirka na kusema kuwa reli inayojengwa nchini ni ya kipekee kuwahi kujengwa Afirka 

“Reli ya kisasa ya Tanzania itakuwa na uwezo mkubwa wa ekseli 35 tofauti na nchi zingine ambazo nyingi ni 25, kwa hiyo itakuwa na uwezo mkubwa wa kubeba mizigo hasa madini kutoka Kongo na Msongati Burundi, pia mwendokasi kwa treni ya mizigo utakuwa 120 na 160 kwa treni za abiria ambayo kitaalamu ni ‘single truck’ hivyo ni tofauti na reli za nchi nyingine”

Mabalozi walipata Fursa ya kupanda treni ya majaribio ya mkandarasi kuanzia stesheni ya Soga hadi eneo la Kikongo mkoani Pwani ambapo mabalozi walifurahishwa na ubora na uimara wa reli ya SGR kwa kuwa hakuna mitikisiko kama ilivyozoeleka katika reli ya ‘Meter Gauge’, katika Safari hiyo Mkurugenzi aliwashukuru Mabalozi hao kwa kuwa anaamini watakuwa wawakilishi wazuri katika kuutangaza Mradi

“Najua mtakuwa mabalozi wazuri kwa nchi mnazofanyia kazi”, alisema Mkurugenzi Mkuu wa TRC.

Akizungumza na waandishi wa Habari Balozi wa Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kuwa Mabalozi ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uchumi wa nchi hivyo uwepo wa Miundombinu imara ya reli, anga, barabara na bandari unaleta matumaini makubwa katika kuleta uchumi imara 

“Tunapotekeleza diplomasia ya uchumi, miundombinu ni lazima hivyo uwepo wangu kwenye treni hii ni ndoto iliyotimia, nampongeza Rais wa Jamhuri na Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kungu Kadogosa kwa usimamizi mzuri” alisema Dkt. Migiro

Halikadhalika Mabalozi pia walitembelea kiwanda cha kutembelea mataruma kilichopo soga kibaha mkoani pwani ambapo kiwanda hicho kinazalisha mataruma 1500 kwa siku na hivyo kipande cha Daresalaam - Morogoro yatatandikwa mataruma yapatao laki tano , mabalozi pia walisifu ubora wa mataruma hayo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa akifafanua jambo kwa  mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC ambao wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.
  Mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC  wakiwa katika picha ya pamoja,wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.
 Baadhi ya Mabalozi wakiwa ndani ya treni ya Wahandisi wakijadiliana jambo
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa akiwaogoza mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC,kushuka kwenye treni ya Wahandisi wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.
 Mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC,wakimisikiliza mmoja wa wahandisi wa ujenzi wa reli hiyo waliposimama kwenye moja ya kituo ili kupata ufafanuzi zaidi,wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.

 Ujenzi wa Reli ya kisasa-SGR ukiendelea kwa kasi
 Mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC,wakisafiri kwa treni ya Wahandisi wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019. 
Mabalozi wakishuka kwenye treni ya Wahandisi wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...