Baadhi ya Wafanyakazi wakiendelea na majuku ya kutengeneza zana za kujengea mradi wa SGR kwenye kiwanda kidogo kilichopo kambi ya Soga, Pwani. 
Mhe. Nahim Azizi Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika akisalimiana na mfanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam akiwa na ujumbe wa mabalozi wengine walipowasili bandarini hapo kwa ziara ya kikazi.

Wakiwa katika Bandari ya Dar es Salaam mabalozi walipata nafasi ya kutembelea mradi wa ujenzi wa upanuzi wa bandari sambamba na kuongeza kina cha bahari ili kuweza kuhudumia meli zinazobeba mzigo mkubwa. 

Mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, Bandari ya Dar es Salaam itakuwa na uwezo wa kuhudumia mizigo ya kiasi cha tani milioni 28 kwa mwaka, ikiwa ni mara mbili ya kiwango cha sasa ambapo inauwezo wa kuhudumia mizigo kiasi cha tani milioni 13 pekee. Aidha, sambamba na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia mizigo mingi, pia mradi huo utapunguza muda wa kuhudumia meli kutoka masaa 80 kwa meli moja kama ilivyo sasa hadi masaa 30 mara mradi huo utakapo kamilika.

Wakati huo huo mabalozi walitembelea mradi wa ujenzi wa wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) ambapo walipata fursa ya kuona maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kuanzia Stesheni jijini Dar Salaam hadi Soga mkaoni Pwani.

Mabalozi wamefurahishwa na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu kwa manufaa ya Wananchi. Mabalozi kwa nyakati tofauti wamesema licha ya miradi hii kuliongezea pato Taifa, mara baada ya kukamilika miradi hii itaiweka Tanzania katika nafasi nzuri zaidi ya ushindani wa kibiashara katika soko la Afrika Mashariki na katika ukanda wa Kusini mwa Afrika
Balozi Ramadhani Mwinyi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni alipoambatana na mabalozi katika ziara ya kikazi Bandari ya Dar es Salaam. 
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza wakati wa ziara ya kikazi Bandari ya Dar es Salaam 
Mabalozi wakifuatilia wasilisho kuhusu mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam 

Mabalozi wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa Shirika la Reli kuhusu mchoro wa mradi mpya wa SGR 
Mabalozi wakipanda Treni tayari kwa safari ya kuelekea Soga mkoani pwani, ambapo pamoja na mambo mengine walijionea kiwanda cha kuunda baadhi ya vifaa vya kujengea mradi 
Sehemu ya mabalozi wakiangalia mandhari yanayozunguka eneo la mradi wa SGR wakiwa njiani kuelekea kambi ya mradi ya Soga 
Sehemu nyingine ya mabalozi wakifurahia jambo wakati wa ziara ya kikazi kutoka stesheni, Dar es Salaam kuelekea Soga, Pwani. 
Sehemu ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioambatana na ujumbe wa mabalozi wakati wa kutembelea mradi wa ujenzi wa SGR 
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara, Shirika la Reli na wafanyakazi wa ujenzi wa mradi wa SGR 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...