Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Imesema, Agosti 9, 2019 (Ijumaa) itatoa uamuzi juu ya pingamizi lililowasilishwa na upande wa Serikali dhidi ya maombi ya askofu Mulilege Kameka kanisa la Boko Yerusalem, ya kuwataka Mwanasheria wa Mkuu na Kamishna wa Uhamiaji wafike mahakamani hapo kujieleza kwa nini wasifungwe kwa kuipuuuza amri ya mahakama.

Uamuzi huo, unatarajiwa kutolewa na Jaji Atuganile Ngwala, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kuhususiana na pingamizi lililowasilishwa na wajibu maombi.

Mwezi Machi Mwaka huu, Mahakama hiyo iliamuru askofu Kameka wa kanisa la wa kanisa la house of prayer shield of faith christian fellowship ( HPSFCFC) lililopo Book Magengeni,

aliyekuwa akishikiliwa na wizara ya mambo ndani ya nchi aachiliwe huru kutoka kizuizini anaposhikiliwa ikisema kwamba uraia wake hauna mashaka.Licha ya kutolewa kwa amri hiyo mpaka leo askofu huyo bado ameshikiliwa na yuko mahabusu gerezani ndio maana ameleta maombi hayo. 

Maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya wajibu maombi ambao ni Mwanasheria mkuu wa serikali (AG) na Kamishna wa Uhamiaji na yalipaswa kusikilizwa leo Agosti 6, 2019 lakini upande wa serikali umewasikisha pingamizi ya awali. 

Katika pingamizi hilo, upande wa serikali ukiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi Jackline Nyantori wamedai kuwa, Kifungu cha sheria ambacho wapeleka maombi wamekitumia kupeleka maombi hayo hakiipi mamlaka Mahakama Kuu ya kuweza kusikiliza maombi hayo .

Akijibu hoja hiyo, wakili wa mpeleka maombi, John Mallya amedai kuwa maombi hayo yameletwa kwa mujibu na taratibu, kwani sheria inaruhusu kuleta maombi ya aina hiyo kwa njia ya hati ya maombi na kiapo kama walivyofanya wao katika kupeleka maombi.

Hata hivyo upande wa serikali umesisitiza kwamba kwa kuwa kosa linalodaiwa kutendeka halikufanyika mbele ya mahakama waombaji walipaswa wapeleke malalamiko hayo kwanza polisi walete madai ndipo mahakama iyasikilize na kuyatolea maamuzi.

Akizungumza nje ya mahakama baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Wakili Mallya amesema Askofu Kameka alikamatwa na Wizara ya Mambo ya Ndani tangu Desemba,2018, ambapo amekaa kizuizini karibia miezi tisa sasa.

"Msingi wa kukamatwa kwake wanadai sio raia, lakini alikuja hapa Mahakama Kuu Machi,2019,ikaamua kuwa Askofu Kameka ni raia na uraia wake hauna mashaka hivyo Magereza na kitengo cha Uhamiaji kimuachie haraka lakini mpaka leo hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji IIvin Mgeta haijatekelezwa ndipo askofu akaleta maombi ya kumshtaki Kamshina Mkuu wa Uhamiaji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili waje waieleze Mahakama kwa nini wamedharau amri halali iliyotolewa na Mahakama .

" Katika maombi yetu tunataka, mahakama iwakute na hatia ya kuidharau amri hiyo, ambapo adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela au mahakama itakavyoona inafaa, pia ni imani kuwa, Mahakama ni nyumba ya haki na tunatarajia kuona haki inatendeka ndio maana tumekimbilia huku tunaamini haki itatendeka,"amesema Mallya.
Askofu wa kanisa la Boko Yerusalem, Mulilege Kameka, akirudishwa mahabusu kutoka Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar ea Salaam, baada ya maombi yake dhidi ya Kamishna wa Uhamiaji na Mwanasheria Mkuu kuahirishwa.
Waumini wa kanisa hilo wakimpungia mkono askafu wao mahakamani hapo baada ya kesi yake kuahirishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...