Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, akizungumza na wanachama wa CCM (hawapo pichani) wa Kata ya Bwisya Tarafa ya Ukara wilayani Ukerewe jana.
………………….


NA BALTAZAR MASHAKA, UKARA

MAKUNDI ya viongozi wasaka vyeo wakiwemo wanachama ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Ukerewe, yaliigharimu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015.Imebainika

Pia wana CCM na wananchi wa Kisiwa cha Ukara na wa Wilaya ya Ukerewe kwa ujumla wao walipokea na kubeba msiba usio wao uliosababisha baadhi ya vitongoji, vijiji,kata na Jimbo la Ukerewe kuangukia mikononi mwa chama wasichokijua undani wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu MKuu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli, alipozungumza kwa nyakati tofauti na wana CCM wa kata nne za Bwisya,Nyamanga, Bukiko na Bukungu kisiwani Ukara.

Alisema kwenye chaguzi za serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa 2015 CCM iliangushwa na makundi ya wasaka vyeo waliokosa kura kutosha, kwenye uchaguzi wa ndani hivyo walinuna na kugeuka makuwadi wa CHADEMA na kusababisha CCM ikapoteza jimbo, baadhi ya kata, vijiji na vitongoji.

Alisema wanachama wa CCM wenyewe waliamua kuwapa kura CHADEMA wakishirikiana na wananchi wasio wana CCM kuuza jimbo kwa kumchagua mgombea wa CHADEMA ambaye hata hivyo alipokosa pa kuzikia msiba huo aliamua kuwaachia mliomsaidia kuubeba na kurejea CCM.

Kalli alidai CCM iliadhibiwa na wanachama wake walioshindwa kwenye kura za maoni kwa msemo wa bora tukose wote akaonya mwaka huu asitokee mtu ambaye kura hazitatosha aseme bora amwage mboga, yeye abaki na ugali, cha moto atakona kwa dhamana waliyo nayo wana CCM ni vitendo si maneno.

Katibu huyo wa CCM Mkoa aliwataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wa Kisiwa cha Ukara pamoja na Wilaya ya Ukerewe kutofanya makosa yaliyopita ya kukumbatia makundi ya wasaka vyeo badala yake washikamane na CCM kwa kuchagua watu wa kuwaletea maendeleo na kuachana na wasaka vyeo.

“Simlaumu Mbunge, kura alizopata wana CCM walimpa wenyewe kwa sababu ya makundi ya wale ambao kura hazikutosha.Walihangaika na kuwa makuwadi wa vyama vingine, mchana walikuwa CCM,jioni NCCR-Magauni (Mageuzi) usiku CHADEMA.Ndiyo yaliyotokea Bukiko Ukara na Ukerewe,”alisema Kalli.

Alisistiza kuwa misiba waliyoibeba ya kuchagua wagombea nje ya CCM ilisababisha Mbunge huyo wa CHADEMA Josephat Mkundi aliuachia msiba huo katikati ya safari baada ya kubaini alidanganywa akajiunga na CCM.

“Nguvu kubwa ya wana CCM ilimsaidia kumbeba Joseph Mkundi kushinda Ubunge Ukerewe lakini kwenye tukio la ajali hakuna kiongozi wa chama chake alishiriki na kujikuta akipwaya.Pia kasi ya maendeleo ya Rais John Magufuli na nguvu kubwa CCM iliyombeba,aliamua kujiunga na timu ya kuleta maendeleo,”alisema Kalli.

Aidha, baadhi ya wana CCM akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Nyamagana walisema kuwa makundi yanayotokana na uchaguzi wa ndani bado yapo ili kushinda lazima makundi hayo yaliyokigharimu Chama 2014 na 2015 yatafutiwe dawa na yavunjwe, kwani tunahitaji maendeleo ili kupiga hatua.
Pia walisema wana CCM si wavumilivu, ni wagumu wa kutafuta kura zingine kutoka nje lakini pia uhusiano duni ndani na nje ya CCM, kuishi kwa kujibagua na kujitenga na jamii ni changamoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...