RAIS wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hana uhakika na kiasi cha fedha anachoidai hakika lakini anaimani kuwa anaidai kwani hata siku chache kabla ya kukamatwa kwake aliikopesha TFF Sh. Milioni 15.

Amedai, alikuwa akiikopesha TFF fedha mara kwa mara kwani wakati anaingia madarakani, shirikisho hilo lilikuwa na hali ngumu kiuchumi iliyosababisha madeni makubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusababisha akaunti za shirikisho hilo kufungwa mara kwa mara.

Malinzi amedai hayo leo Agosti 13, 2019 wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde, dhidi ya kesi inayomkabili ya mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha baada ya kukutwa na kesi ya Kujibu.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi Richard Rweyongeza amedai, alikuwa akiikopesha TFF fedha zake binafsi na alikuwa akifanya hivyo kupitia akaunti waliyoifungua kati yake na shirikisho hilo.

Amedai kiasi hicho cha sh. Milioni 15, zilikuwa ni kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kufuzu fainali za Afrika kati ya Tanzania na Lesotho 

Amedai akiwa Rais, alihakikisha shughuli mbalimbali za timu zinakwenda hadi kushiriki michuano mbalimbali ya kimataifa ambapo ili kufanikisha hilo, mara nyingine ilikuwa ikinilazimu kutumia fedha zangu za mfukoni ili kuweza kuinusuru TFF hali ikiwa nzuri narudishiwa na wakati mwingine kukopa kwenye kamati tendaji na kwa watu binasfi" alidai

Malinzi alidai kuwa aliikopesha TFF kutokana na hali ngumu ya kifedha iliyokuwa ikiikabili na hivyo kulazimika kutumia fedha zake binafsi, kukopa kwa watu binafsi ama kamati ya utendaji ili kunusuru hali hiyo hasa katika matukio muhimu yanayoikuta TFF na timu ya Taifa Taifa Stars.

Akiendelea kutoa utetezi wake, amedai, baadhi ya matukio ambayo alilazimika kutoa fedha zake na kuikopesha TFF mojawapo ni ile ya kulikomboa basi la TFF ambalo lilikuwa linashikiliwa na kampuni ya udalali ya Yono kufuatia amri ya mahakama la kuilipa Kampuni ya Pachi Line iliyokuwa ikitoa huduma za tiketi uwanjani.

Ameendelea kudai kuwa, aliilipa sh milioni 20 kwa kampuni ya udalali ya Yono ambapo TFF ilikuwa ikidaiwa na TRA na walitaka kukamata basi ambalo lilitolewa na wafadhili wao, Kampuni ya Bia ya TBL,Pia alilipia sh.milioni 40 za tiketi za ndege Kampuni ya Ethiopia Airline, za wachezaji wa Tàifa Stars waliokuwa wanakwenda Nchini Nigeria katika Mashindano ya Afrika yaliyokuwa yakufuzu Misri

Aidha ameongeza kudai kuwa aliwahi kuikopesha TFF USD 7000 wakiwa Harale, Zimbabwe baada ya wachezaji waTaifa Stars kutolewa mizigo yao nje ya hoteli waliyokuwa wamefikia kwa sababu Shirikisho la mpira Zimbabwe lilikuwa likidaiwa na hoteli hiyo, hata baadhi ya mashahidi waliowahi kutoa ushahidi mahakamani hapa walithibitisha hilo akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa TFF Daniel Masangi"alidai Malinzi

Amewataja mashahidi wa upande wa mashtaka waliodhibitisha jambo hilo Mahakamani akiwemo Katibu Mkuu Wilfred Kidao, Hellen Adam na Sareki Yonasi.Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF Nsiande Mwanga, Karani Flora Rauya na Selestine Mwesigwa
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya uwamuzi wa kupokelewa kwa kielelezo cha nyaraka ya taarifa ya madeni kati ya TFF na Malinzi ama laKesi hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...