Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea vielelezo viwili ambavyo ni taarifa ya benki ya mwaka 2014 na risiti 13 zilizoonesha TFF ilikuwa ikimlipa Malinzi fedha za mkopo alizokuwa anawadai.

Katika utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde, Malinzi ameithibitishia mahakamani hapo kuwa anakumbuka alikuwa anaidai TFF zaidi ya Sh milioni 152.6.

Akiongozwa na wakili Richard Rweyongeza kutoa ushahidi wake Wa utetezi Malinzi amedai kuwa, katika taarifa ya benki ya Januari 2014 hadi Agosti 19, 2014 alikuwa anaidai TFF zaidi ya sh. Milioni 152 huku kiasi cha USD 5000 ambazo anadai kuzitoa nchini Msumbiji hazikuingizwa kwenye mfumo huo badala yake waliingiza kwa mkono.

Ameendelea kudai kuwa, fedha hizo zilipobadilishwa kuwa fesha za kitanzania jumla ilikuwa yake ilifikia Sh milioni 8.3 ambapo kwenye taarifa hiyo ya benki waliandika kuwa ‘’kiasi unachotudai kwa mujibu wa kumbukumbu zetu ni Sh 152,613,004.83.’’

Amedai kuwa alipokuwa analipwa baadhi ya fedha walikuwa wakimpa risiti kwa majina yake na kwamba aliendelea kutoa fedha kwa TFF hadi alipokamatwa mwaka 2017.

Amedai kuwa, miongoni mwa risiti alizonazo zilisainiwa na mhasibu wa TFF Hellen Adam ambaye alikuwa shahidi wa kumi wa upande wa mashitaka na zingine zilisainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Daniel Msangi ambaye alikuwa shahidi wa sita huku risiti nyingine haikuwa na saini lakini kwenye taarifa ya benki ilionesha imeingizwa kama mkopo.

"Risiti zote za TFF zinatunzwa na idara ya uhasibu ya shirikisho hilo na kwamba nilikuwa nikilipwa kwa mafungu mafungu kutokana na hali ya shirikisho hilo kuwa mbaya kiuchumi ambapo idara ya fedha ilikuwa ikikaa na kuangalia namna ya kumlipa kutokana na kile wanachokipata”

Malinzi alidai mwaka 2015 hali ya TFF ilikuwa haijabadilika kwani alikuwa akitoa fedha zake mfukoni na kuwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuchangia na mwishoni mwa mwaka 2014 alijenga Ofisi ya Rais na nyaraka alizokuwa anatunza nyumbani alihamishia kuzitunza ofisini.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, mwaka huu kwa ajili ya utetezi.

Mbali na Malinzi, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya ambapo wote hao wanakabiliwa na mashitaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...