Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Idara ya Uhamiaji nchini imewapandisha vyeo maafisa 513 katika ngazi mbalimbali wakiwemo Marakibu Waandamizi kuwa Makamishina Wasaidizi wa Idara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuwapandisha vyeo Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji alisema kuwa kupandishwa vyeo ni kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi.

Alisema kuwa kupanda kwa vyeo huko sio ndio tiketi ya moja kwa moja kwa moja kwani wanaweza kupanda au hata kushushwa kwa vyeo hivyo.Chogero alisema maafisa hao wamekaa kwa muda mrefu bila kupanda hivyo wengine ambao hawajapanda waendelee kujituma katika kazi.

Pia alisema kuwa Makamishina Wasaidizi wawasimamie waliochini yao.
"Mmepandishwa vyeo lakini vinaweza kushuka kutokana na kutokwepo kwa mabadiliko ya kupanda kwa vyeo kifikra na kiutendaji." Alisema chogero

Alisema kuwa vyeo vinahitaji uwajibikaji wa matokeo chanya katika idara ya Uhamiaji katika utoaji huduma bora kwa Wananchi.Naye Kamishina Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyepanda cheo Novaita Mrosso alisema kuwa hawatawaangusha wenzake waliopanda cheo katika utumishi wa Idara hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji akimvisha cheo cha Kamishina Msaidizi James Mwanjotile awali alikuwa na cheo Mrakibu Mwandamizi wa Idara hiyo katika katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji akiwa katika picha ya pamoja na Makamishina wasaidizi mara baada ya kupanda cheo hicho katika katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero akizungumza na maafisa wa Idara ya Uhamiaji waliopandiswa Vyeo katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
Kamishina wa Udhibiti wa Mipaka Samuel Mahirane akizungumza katika kuwaasa maofisa wa Idara ya Uhamiaji waliopandiswa Vyeo katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.

Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Novaita Mrosso akitoa neon la shukrani kwa niaba ya waliopandishwa vyeo mbalimbali Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...