Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAOFISA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wameendesha ukaguzi wa kushtukizwa kwenye magodauni ya kuuza vifaa vya ujenzi jijini Dar es  Salaam na kubaini kuwepo kwa baadhi ya nondo zinazozalishwa na baadhi ya viwanda nchini zisizokidhi viwango vya ubora viliwekwa kwa mujibu wa sheria.

Ukaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika magodauni ya kuuza nondo yaliyopo Buguruni, Mbagala, Kariakoo na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi huo mwishoni mwa wiki, Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ramadhan Shija, alisema hatua hiyo unalenga kujiridhisha kama wazalishaji wa nondo viwandani wanafuata matakwa ya viwango husika pamoja na kutoa elimu kwa umma.

Shija, alisema ukaguzi wao umebaini baadhi ya nendo ni fupi kulingana na kiwango husika. "Nondo nyingine tumebaini kuwa ni fupi, kwani badala ya kuwa na urefu wa futi 38 zina urefu wa futi 37.6, hivyo kuna udanganyifu unaofanyika," alisema Shija.

Kwa upande wake Mkaguzi Mwandamizi wa TBS, Donald Manyama, alisema 
ukaguzi wao ulilenga urefu wa nondo na kipenyo. Alisema kupitia ukaguzi wao wamebaini baadhi ya nendo zinafikia kipenyo husika na zingine hazifikii. Kwa mujibu wa Manyama baada ya kubaini kasoro hizo kazi inayofuata ni kwenda kwa wazalizaji na kuwaeleza kuhusiana na kasoro walizobainia ili wazirekebishe vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria. Pia Manyama alisema kasoro walizobaini kwenye baadhi ya nondo zinawasukuma kufanya ukaguzi huo nchi nzima na kutoa elimu kwa umma, umuhimu wa kuhakikisha bidhaa wanazotaka kununua zinakidhi vigezo kwa kuoneshwa nyaraka husika na wazalishaji au kufika ofisi za shirika hilo kupata ushauri.

Aliongeza kwamba wanafanya hivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata 
bidhaa wanazokusudia kulingana na mahitaji. alitaja madhara ya nondo 
hizo kutokidhi viwango kuwa ni pamoja na majengo kuweza kuanguka.
Alifafanua kwamba ukaguzi huo ni sehemu ya taratibu wa TBS kwa sababu 
wakishatoa leseni kwa mzalishaji mbali na kufanya ukaguzi kwenye eneo 

za uzalishaji kwa kushtukiza pia ununua sampuli za bidhaa katika masoko bila mzalishaji kuwa na taarifa na kwenda kuzipima kwenye maabara za shirika ili kujiridhisha kama anaendelea kufuata viwango. 
Zinapokuwa na kasoro mzalishaji anatakiwa kuzirekebishe au kutakiwa kuziondoa bidhaa hizo sokoni na kuziteketeza gharama zake pamoja na hatua nyingine za kisheria.

Meneja mauzo wa kampuni ya vifaa vya ujenzi la 92, Emmanuel Marongo, 
alipongeza utaratibu huo wa TBS akisema unalenga kuwawezesha wananchi 
kununua bidhaa zenye ubora kulingana na makusudio yao.

Alisema hata wao mteja akienda kununua aina fulani ya bidhaa wanamsaidia kumpa elimu ili aweze kununua bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji yake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya 92 ya jijini Dar es Salaama wakisaidiana na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania TBS (hawaonekani pichani) kupima viwango vya nondo. Maofisa hao walifanya ukaguzi wa kushtukiza mwishoni mwa wiki katika magodauni mbalimbali. Picha Chalila Chibuda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...