Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania nchini, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akiwa na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo pamoja na warembo hao (waliosimama) leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii, ambapo ameeleza kuwa maandalizi yapo tayari na mashindano yatakuwa ya aina take, leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa shindano la Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) Basila Mwanukuzi Shayo amesema kuwa fainali za mashindano hayo yatahitimishwa rasmi siku ya ijumaa, Agosti 23 huu katika ukumbi wa Millenium Tower LAPF uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwanukuzi amesema kuwa washiriki wapatao 20 kutoka Mikoa mbalimbali nchini wapo kambini tangu Agosti 12 wakijiandaa na kinyang'anyiro cha kuwania taji hilo.

"Kufanyika kwa fainali hizi ni hitimisho ya mashindano ya Mikoa ambayo yalifanyika kuanzia mwezi April mwaka huu" ameeleza.

Ameeleza kuwa kwa kipindi walichokuwa kambini washiriki wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutembelea, kuwafariji na kucheza michezo mbalimbali na watoto katika kituo cha watoto yatima kilichopo Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam  pamoja na kufanya shughuli nyingine za kijamii.

"Washiriki wakiwa kambini pia walipata nafasi ya kufanya mashindano madogo madogo kwa mujibu wa mashindano ya dunia ambapo walifanya mashindano ya kumtafuta mrembo mwenye kipaji, mrembo mwenye mvuto katika picha, mrembo mwanamitindo, mrembo mwanamichezo na mrembo chaguo la watu, na washindi watatangazwa siku ya tukio" ameeleza Mwanukuzi.

Mashindano hayo yanategemewa kuwa ya aina yake ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kujipatia tiketi zao ili waweze kumshuhudia mlimbwende ambaye ataliwakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya dunia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...