Na Ripota Wetu, Michuzi Blogu

MBUNGE Jimbo la Manonga lililopo Igunga mkoani Tabora Seif Gulamali amempongeza Rais John Magufuli kwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kuufanikisha kuumalizika vema kwa mkutano mkuu wa SADC uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari kwa nyakati tofauti Gulamali amesema anampongeza Rais Magufuli na watanzania wote kutokana na lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa moja ya lugha itakayotumiwa katika mikutano ya SADC, suala alilosema litazidi kulitangaza taifa la Tanzania.

Amesema kitendo cha Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa SADC katika mkutano huo kunazidi kuiletea heshima Tanzania ambayo tangu ilipopapata uhuru wake mwaka 1961 imeendelea kuwa kitovu kikuu cha amani miongoni mwa mataifa ya Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla. 

"Pamoja na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, pia mkutano huo wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ulifana chini ya uenyeji wake na hotuba yake ikigusia maeneo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya jumuiya hiyo.

"Jambo hili litazidi kuhimarisha umoja na mshikamano wa nchi hizo kama alivyokuwa ameligusia katika hotuba yake alipokuwa akifunga mkutano huo,"amesema.

Mbunge huyo amesema kauli ya Rais Magufuli kueleza kuwa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa wanachama wa SADC ili kuharakisha jitihada za kuleta maendeleo fungamani, linaonesha ni kwa namna gani kiongozi huyo ana kiu ya kuziona nchi zote zilizomo ndani ya SADC zinapiga hatua zaidi za kimaendeleo kama alivyo na kiu hiyo kwa Tanzania .

Amesema pamoja na kuzitaka nchi wanachama kutoa kipaumbele katika suala zima la usalama, amani na utulivu pia alizitaka kuboresha eneo la ukuaji wa viwanda, biashara na utengenezaji wa fursa za kibiashara.

Hili ni jambo muhimu katika uzalishaji wa ajira na maendeleo yake na wananchi kwa ujumla.Ukweli anastahili pongezi kwa kuliona hilii,"amesema Gulamali.

Ameongeza kimsingi mambo mengi ambayo Rais Magufuli amegusia katika hotuba yake hiyo yanaakisi yale anayoendelea kuyafanya hapa nchini ambayo kwa kiasi kikubwa matokeo yake yanaonekana kwa kadri siku zinavyozidi kwenda.

Pia amesema hatua ya Rais Magufuli kuzitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuweka mkazo katika usimamizi wa rasimali zake una maana kubwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.

Kuhusu lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa miongoni lugha rasmi ya nne kutumika SADC, Mbunge huyo amesema ni fahari kwa Tanzania kwani itazidi kulitangaza Taifa na kuzidi kuliletea heshima.

"Tunaamini lugha ya Kiswahili itaendelea kuzungumzwa na nchi nyingi duniani kama ambavyo tumeshuhudia nchi kadhaa zinazungumza lugha hii adhimu,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...