MBUNGE wa Jimbo la Temeke Jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea ametoa rai kwa vijana nchini ikiwa ni katika kilele cha maadhimisho siku hii ya vijana ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Agosti 12 kila mwaka ambapo amewaasa vijana hao kuacha kutumika vibaya katika nyanja mbalimbali huku akiwataka waweze kujitambua na kuzitumikia nafsi zao kwa faida zao binafssi na si kutumika.

Mbunge huyo wa Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema hayo jana katika kongamano lililoandaliwa kwa mara ya kwanza na Taasisi Open Mind ambayo iko chini ya Mwenyekiti Abel Otieno ambaye pia ni maarufu kwa jina la 'MC Rhevan',lililowakutanisha vijana na wasajasiriamali lililofanyika katika hoteli ya Lamada Jijini Dar es Salaam.

Aidha Mtolea amesema kuwa vijana wengi wamekua hawana elimu ya kujitegemea hasa katika kujiajiri na kujiwekea malengo ya kuweza kupata ajira binafsi huku akiwataka vijana kuangalia nchi inakwenda kwapi ili wasiweze kuachwa njiani huku akiwataka vijana wajifunze kutenda mambo kwa viyendo kuliko kuwa wazungumzaji zaidi ili mwisho wa siku jamii iweze kuyaona matunda ambayo yamezalishwa na vijana wake.

"Usipojitumia kama wewe mwenyewe kijana basi wenzako waliokuzunguka watakutumia sisi wanasiasa tutakutumia na watu wengine watakutumia sababu watu wengi wanapenda kuwatumia vijana kwakuwa ndiyo kundi kubwa ambalo mtu akilitumia ataweza kufanikisha jambo lake hivyo tambueni kuwa mwisho wa siku unayoyafanya leo ndiyo utakayovuna kesho"alisema Mtolea.
 Aidha Mwenyekiti wa Taasisi ya Open Mind MC Rhevan amesema Taasisi hiyo watakua wakiandaa makongamano ya vijana ili kuweza kuamsha ari na kutoa elimu kwa vijana kila mwezi huku wakiwa wanazunguka n katika mikoa mbalimbali ambapo mwezi ujao wataanza na Jimbo la Temeke kwa kutoa elimu ya kujitambua, afya na namna matumizi ya fedha ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za ujasiriamali na elimu ya uwekezaji kwa sababu vijana wengi bado hawajapata fursa ya elimu hiyo ili pindi inapotokea fursa ya kuwekeza katika nyanja yeyote ile vijana hao waweze kuchangamkia fursa hiyo baada ya kupatiwa elimu na mafunzo hayo bila bila malipo yeyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...