JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) imesema ipo kwenye mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa kanda kwa ajili ya kusaidia nchi wanachama wa jumuiya hiyo. 

Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2019 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa jumuiya hiyo Domingos Gove wakati anazungumza na waandishi wa habari za mikutano ya SADC inayoendelea jijini. 

“Kwa sasa tupo katika mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa pamoja wa kikanda ambao lengo ni kuhakikisha tunasaidiana katika chakula kwa nchi za SADC,” amesema Gove. 

Amefafanua katika mkakati huo pia watahakikisha kunakuwa na miundombinu itakayofanikisha nchi wanachama zinajikita kwenye kilimo kwa ajili ya kupata chakula cha kutosha kwa nchi zao. 

Mkurugenzi huyo wa Kilimo,Chakula na Maliasili ameongeza kuwa kwenye mfuko huo ambao utaanzishwa kwa nchi za SADC utahakikisha kunakuwa na usambazaji wa mbegu bora zisizo na magonjwa , upatikanaji wa soko kwa malighafi zinazohusika kwenye suala la kilimo. 

Pia amesema mikakati mingine ni kuongeza ushindani na uzalishaji wa nafaka pamoja na kuhakikisha kunakuwa na sera ya kulinda usalama wa chakula. 

“Tumejipanga kuhakikisha kupitia mfuko huo wa kilimo tunazalisha chakula kwa wingi na pale ambapo nchi mojawapo itakuwa na tatizo la uhaba wa chakula basi tunasaidia kupeleka chakula kutoka kwenye nchi zenye chakula cha ziada,”amesema. 

Ameongeza vyakula ambavyo vitazalishwa pamoja na mambo mengine vitazingatia suala la lishe kuhakikisha walaji wanakuwa na afya njema na imara kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo kwa nchi wanachama. 

Wakati huo huo jumuiya hiyo imeeleza namna ambavyo imejipanga kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo zinakuwa na miundombinu ya uhakika. 

Ambapo kwenye eneo hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Habari, Matangazo na Machapisho Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya SADC Zamarad Kawawa ametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo Serikali ya Tanzania ilivyoweka mkazi katika ujenzi wa miundombinu. 

“Tanzania tuko vizuri, katika eneo hilo, ukienda bandarini, viwanja vya ndege , reli, na barabara kote kumeimarika kwa kiwango kikubwa,”amesema Kawawa ambaye pia nia Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO).

 Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa Jumuiya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),Domingos Gove akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari za SADC,kuhusu  mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa pamoja wa kikanda ili kuhakikisha nchi hizo zinasaidiana katika chakula kwa nchi za SADC.
  Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa Jumuiya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),Domingos Gove  akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), wanaoandika habari za SADC leo Katika moja ya Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Habari, Matangazo na Machapisho Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya SADC, Zamarad Kawawa akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari za SADC,leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar,ambapo alieleza namna ambavyo Serikali ya Tanzania ilivyoweka mkazo katika ujenzi wa miundombinu. 
Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa Jumuiya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),Domingos Gove amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati wa kuanzishwa mfuko huo wa kilimo  ambao kwa nchi za SADC, utahakikisha kunakuwa na usambazaji wa mbegu bora zisizo na magonjwa , upatikanaji wa soko kwa malighafi zinazohusika kwenye suala la kilimo. Picha na Michuzi JR.
Waandishi wa habari wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri  ukumbini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...