Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

RAIS Dkt. John Joseph Magufuli amesema kuwa milango ya uwekezaji nchini ipo wazi na wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini wanakaribishwa kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ili kuleta ukombozi wa kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika jukwaa la wafanyabiashara baina ya Afrika Kusini na Tanzania Rais Magufuli amesema kuwa wawekezajj wanakaribishwa nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali kwa kuwa nchi Ina hazina ya rasilimali za kutosha zikiwemo pamba na kahawa na hata sekta ya viwanda hasa vya dawa mbalimbali jambo ambalo ni changamoto kubwa katika ukanda wa SADC.

"Ukanda wa SADC una changamoto kubwa katika sekta ya usambazaji wa madawa, Tanzania tunatumia zaidi ya shilingi bilioni 270 katika kununua dawa na vifaa tiba na zaidi ya asilimia 90 ya dawa zinazosambazwa na bohari ya dawa zinatoka nje hivyo hatuna budi kuelekeza nguvu kwenye ukombozi wa kiuchumi hasa kwa kuangalia masuala ya uwekezaji na biashara" ameeleza Magufuli.

Aidha amesema kuwa Afrika Kusini na Tanzania ni washirika wazuri katika masuala ya biashara na lazima nchi hizo zipambane na changamoto ya uzalishaji ambayo bado ipo chini na hiyo ni kwa kuanzisha viwanda vyao wenyewe ambavyo vitachakata malighafi zinazozalishwa ndani ya nchi hizo na sio kusafirisha malighafi hizo nje ya nchi hali inayopelekea kupoteza ajira nyingi.

Kwa upande wake Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameanza hotuba yake kwa kutoa pole kwa watanzania kufuatia ajali ya moto iliyotokea Mkoani Morogoro na kupoteza maisha ya watanzania zaidi ya 70, na amewaombea manusura wa janga hilo waweze kupona haraka, pia ameishukuru Tanzania kwa kuwa washirika wazuri wa kibiashara na kubwa zaidi ni kushirikiana nao katika kipindi cha kupigania Uhuru kwa kutoa mafunzo, makazi, ushirikiano na umoja walioonesha kipindi kile hadi sasa.

Ramaphosa amesema kuwa amani tuliyonayo tuitunze kwa gharama yoyote na hiyo ni pamoja na kuimarisha umoja na kupiga vita masuala ya rushwa pamoja na kuimarisha biashara hasa kwa kutengeneza mazingira wezeshi ya kibiashara kwa kutoa elimu na ujuzi ambao unaenda sambamba na mazingira yetu.

Aidha ameshauri kuwatengeneza vijana kwa manufaa ya baadaye na hiyo ni pamoja na kuwapa ujuzi na teknolojia hasa katika masuala ya uchumi, biashara na viwanda ili kwenda sambamba na soko la dunia ambalo Lina changamoto ya ushindani na hiyo ni pamoja na kushirikiana baina yao kwani wasipokuwa na umoja hawawezi kuyafikia maendeleo.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli akizungumza katika Kongamano la jukwaa la wafanyabiashara Tanzania na Africha kusini ambapo amesisistiza nchi za Tanzania na Afrika Kusini zijikite katika kuendeleza na kuimarisha mazingira ya ujenzi wa viwanda ili kutengeneza ajira na kuacha kuuza bidhaa ghafi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...