MPANGO kazi wa kuendeleza Miji Tanzania umezinduliwa jana Jijini hapa, huku Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Seleman Jafo akiwataka Wakuu wa Mikoa kuusimamia mpango huo.

Akizindua jana Jijini hapa,Jafo aliwataka Wakuu wa Mikoa nchini kuusimamia mpango huo ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo."Niwaombe wadau tujipange kwenda kutekeleza mpango huu na niwaombe,Wakuu wa Mikoa kuanisha eneo kwa eneo ikiwa ni pamoja na kuusimamia," alisema.

Jafo alisema kwa sasa ongezeko la watu ni kubwa hususan katika Mikoa ya Dodoma na Dar es salaam hivyo akadai kwamba umekuja wakati muafaka.
"Bila kuwa na mpango kazi inawezekana tukaishi maisha sio azuri,mabadiliko haya ambayo yanafanywa sasa hivi ni muhimu sana katika upangaji wa miji," alisema.

Waziri Jafo alisema Mji wa Dar es salaam upo hovyo na haujapangika vizuri hivyo akataka isitokee tena kwenye miji mingine."Mji wa Dar upo hovyo,hata moto ukitokea hauwezi kuokoa tujiulize ni majanga mangapi yametokea tumeshindwa kuokoa sababu ya Miji kupangwa vipaya ?

" Jiji la Dar tumechelewa yaani unatamani uchukue Greda uvunje nyumba kwani zimekaa vibaya.Niwapongeze Dodoma angalau Jiji limekaa vizuri,"alisema Jafo.Aidha,alisema lazima Miji ipangwe vizuri kwani kwa sasa ile ambayo imepangwa vizuri imeweza kusababisha kuongezeka kwa mapato kutokana na Serikali kuweza kukusanya kodi.

"Sehemu zingine gari la zimamoto haliwezi kupitia,sehemu zingine kupitisha jeneza shida,msiba unakuwa nyumba ya tatu sababu kwenye msiba hakufikiki.Kuna vijana wana magari mazuri lakini yanakaa kwa jirani wanapokaa hakufikiki," alisema.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angelina Mabula alisema mpango huo ni muhimu na utasaidia katika ujenzi wa Miji iliyopangika pamoja na kuongeza thamani ya ardhi.

Mabula alisema Serikali imetayarisha Mipango kabambe 30 kwa mwaka 2018-2019 ambapo 20 imekamilika huku 10 ikiwa katika mipango mbalimbali.

Naye,Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Fedha na Mipango,Adolf Ndunguru alisema kwa sasa Miji inakuwa hivyo mpango huo umekuja wakati muafaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...