Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi akiangalia kiatu kwa ajili ya majeshi akiwa katika banda la Tantrade lililopo kwenye maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi za SADC.Kulia ni Mkurugenzi wa Tantrade Edwin Rutageruka. Picha na Michuzi Jr
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi (kushoto) akipata maelezo kwenye banda la Shirika la Ndege Tanzania lililopo kwenye wiki ya nne ya maoenesho ya viwanda kwa nchi za SADC yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea banda katika maonesho ya wiki ya nne ya viwanda kwa nchi za SADC
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi akiwa kwenye banda la Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) baada ya kutembelea banda la wakala hao kwenye maonesho ya wiki ya nne ya viwanda kwa nchi za SADC.

Na Leandra Gabriel ,Michuzi TV

MKURUGENZI wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi leo Agosti 7, ametembelea maonesho ya nne ya wiki ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, viwanja vya Karimjee na Gymkhana jijini Dar es Salaam na kuwashauri watanzania kuzidi kutembelea maonesho hayo ili kuweza kupata huduma, ujuzi na maarifa yanayotolewa na taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika maonesho hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea maonesho hayo Dkt. Hassan amesema kuwa maonesho yanaendelea vyema ni nafasi kwa wananchi kutembelea viwanja elekezi bure bila malipo ili kuweza kupata masoko ya uhakika pamoja na kubadilishana ujuzi.

Amesema kuwa wiki ya viwanda itafungwa rasmi kesho na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein na majadiliano na mikutano mbalimbali ya wanajumuiya ya SADC itaendelea.

Dkt. Abassi amesema kuwa kuanzia tarehe 9 hadi 12 wiki ijayo maafisa waandamizi (makatibu wakuu) kutoka jumuiya ya SADC watakutana kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo na tarehe 13 na 14 kitafanyika kikao Cha mawaziri wa nchi za SADC ambapo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki profesa. Palamagamba Kabudi atapokea kijiti cha uenyekiti wa baraza la mawaziri wa nchi za SADC.


Vilevile amesema kuwa kuanzia tarehe 15 wageni mbalimbali wataanza kuingia nchini na tarehe 17 na 18 mkutano mkuu wa 39 wa wakuu na Serikali kwa nchi 16 za jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika utafanyika ambapo Rais Magufuli atapokea kijiti cha uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa muda wa mwaka mmoja kutoka nchini Namibia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...