Muasisi na Mlezi wa Shirikisho la Familia kwa Ajili ya Amani ya Dunia, Dkt. Hak Ja Han Moon, kutoka Korea anataraiwa kuwasili nchini kwa ajili ya kushiriki tamasha ambalo mgeni rasmi inatarajiwa awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya Kiongozi Mkuu wa Shirikisho hilo nchini, Stylos Simbamwene, Semeni Kingaru amesema tamasha hilo la Baraka na Upendo, litafanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam 31 mwezi huu.

Ujio wa Dkt. Moon utaambatana na wageni wapatao 200 kutoka Korea, Japani, China, Marekani na Uingereza ambapo timu ya maandalizi imeanza kuingia nchini juzi na jana huku wageni 200 wakitarajiwa kuwasili nchini 26 Mwezi huu.

“Watapokewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, na kwenda kutembelea mbuga ya wanyama Mikumi, kabla ya Muasisi wa Shirikisho kuwasili na kujiunga nasi kati ya tarehe 28 na 29 mwezi huu,” amesema Kingaru.

Amesema shughuli mbalimbali zitakazofanyika kwenye tamasha hilo zimejikita katika Dira ya Shirikisho ambayo ni kudhibiti mmomonyoko wa maadili. ili kuijenga Tanzania ya kizalendo.

Amesema tamasha hilo litakalojumuisha wanandoa 80,000 linatarajiwa kuripotiwa mubashara na vyombo mbalimbali vya habari nchini, ingawa hakuvitaja. 

Kwa upande wa maandalizi ya tukio hilo nchini, yapo chini ya uratibu wa kiongozi mkuu kitaifa wa Shirikisho hilo, Simbamwene na viongozi wenzake, Kingaru na Neema Elpin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...