Na Sophia Mtakasimba

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali wanaendesha zoezi la kuwapima vinasaba majeruhi ambao hawajitambui wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro ili kubaini ndugu zao halisi.

Katika taarifa aliyoitoa katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa hospitalini hapo Bw.Aminiel Aligaesha alisema kuwa awali hospitali ilitoa wito wa ndugu kujitokeza kutambua majeruhi, lakini walijitokeza ndugu zaidi ya mmoja kwa majeruhi mmoja.

“Hii imeleta mkanganyiko hivyo tumeona tushirikiane na wenzetu wa Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili wachukue vinasaba vya wagonjwa na kulinganisha na ndugu waojitokeza ili kuhakikisha kwamba zoezi hili haliingii dosari,” alisema Bw.Aligaesha .

Kuhusu hali za majeruhi wa moto Bw. Aligaesha alisema kuwa kati ya majeruhi 46 waliopokelewa, 8 wamefariki dunia, 13 wapo katika wodi ya mahitaji maalumu na hawajitambui, 25 wanajitambua na wapo katika wodi za kawaida ambapo madaktari na wauguzi wanaendelea kuwapa huduma nzuri ya daraja la kwanza.

Akifafanua aina ya ndugu wanaohitaji kuchukuliwa vinasaba kwa ajili ya utambuzi Meneja wa Maabara ya Vinasaba kutoka Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bi. Hadija Said Mwema alisema ndugu wanaohitajika kulinganishwa vinasaba kwa urahisi ni wazazi wawili au watoto wa majeruhi. 

“Kwa wale ambao kwa bahati mbaya wazazi walishatangulia na hawakubahatika kuwa na watoto hapo sasa tutaomba ndugu wa karibu kwa mfano Kaka, Dada au Baba mdogo, lakini kitaalamu ningependa wananchi wafahamu kwamba urahisi wa ulinganifu ni kwa ndugu wa karibu,” alisema Bi. Hadija.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Bw.Aminiel Aligaesha akiongea na waandishi wa habari kuhusu utambuzi wa ndugu wa majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Kulia ni Meneja wa Maabara ya Vinasaba, Bi.Hadija Said Mwema kutoka Mamlaka ya Mkemia mkuu wa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...