Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA mkuu wa Timu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema kwa msimu huu ameweza kusajili wale wachezaji aliowataka hususani katika safu ya ushambuliaji.

Zahera amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Kariobang Sharks uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.

Amesema, anaanini kuelekea msimu ujao wa 2019/20 kikosi chake kitakuwa ni bora zaidi ya msimu uliopita na watakuwa kwenye mwendo wa mchakamchaka kwani hakuna mchezaji atakayekuwa anatembea uwanjani. 
Zahera amesema ushindani msimu ujao ni mkubwa naye amejipanga kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani mkubwa msimu ujao.

"Nimefurahi kuona mashabiki wengi wamejitokeza leo uwanja wa Taifa, hichi ni kitu ambacho tulikikosa msimu uliopita hivyo msimu ujao waendelee kujitokeza kwa wingi."Kazi yetu msimu ujao itakuwa ni kote kwani hatuna mchezaji atakayekuwa anatembea wote wanakimbia mwanzo mwisho," amesema.

Kwenye mchezo huo, Kariobangi Sharks waliweza kutangulia kwa kufunga bao dakika ya 48 kupitia kwa Patrick Otieno na baada ya dakika tisa, Yanga wanasawazisha kwa mkwaju wa Penati kupitia kwa Patrick Sibomana dakika ya 57.

Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa na Ushindani mkali kwa kila timu kutafuta matokeo, Yanga wametengeneza nafasi nyingi kupitia kwa Patrick Sibomana ambaye amekuwa ni moto wa kuotea mbali kipindi cha kwanza akicheza vizuri na mshambuliaji kutoka Namibia Sadney Urikhob.

Kabla ya mchezo huo kulitanguliwa na mechi kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva, Maveteran wa Yanga na Maveteran wa Pamba.Pia, walitumia siku ya leo kutambulisha wachezaji wao wapya waliosajiliwa msimu huu pamoja na jezi zao.

Mashabiki wa Yanga waliweza kujitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kubeba watu 60,000.ni kama wote uwanja wa Taifa leo kwenye kilele cha Mwanachi.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Farouk Shikhalo, Moustafa Selemani, Muhaeami Issa ‘Marcelo’, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Mohammed Issa ‘Banka’/ Mrisho Ngassa dk65, Sadney Urikhob/ David Molinga ‘Falcao’ dk87, Juma Balinya/ Maybin Kalengo dk82 na Patrick Siebomana.

Kariobangi Sharks: Brian Bwire, Eric Juma/David Simiyu dk82, Samuel Qlwande, Kyara Amani, Nixon Omandi, Yidah Sven, Shaphan Oyugi/James Mazembe dk59, Harrison Mwendwa, Patrick Otieno/ Julius Masaba dk54/Peter Oudo dk88, Patrick Nguyi na Erick Kapato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...