Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Botswana, Jan SADEK walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo baina yao yalijikita kwenye masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Sambamba na hayo katika mazungumzo hayo Dkt. Ndumbaro aliendelea kumueleza Balozi Jan, juu ya umuhimu wa Umoja wa Ulaya kutekeleka wito alioutoa Rais Magufuli wakati wa Mkutano wa SADC kuhusu kuiondolea nchi ya Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi. Balozi Jan alikuwa nchini kuhudhuria Mkutano wa SADC.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Jan. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akisisitiza jambo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Jan. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...