Charles James, Michuzi TV

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amefanya ziara ya ukaguzi katika kiwanda cha HONG WEI INTERNATIONAL kilichopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na kuagiza kufanyika uchunguzi katika usahihi wa malipo ya mishahara ya Wafanyakazi iliyoandikwa kwenye mikataba na kiasi halisi kinachopokelewa ambapo imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Serikali ikawa inapoteza mapato ya kodi ya mshahara.

Naibu Waziri Mavunde amevitaka vyombo vya uchunguzi kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mufindi kujiridhisha na nyaraka mbalimbali za mishahara ya wafanyakazi na kuwasilisha taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ndani ya siku saba.

Wakati huo huo,Naibu Waziri Mavunde amekitaka Kiwanda hicho kuwapa Wafanyakazi wote mikataba kwa mujibu wa Sheria na.6/2004 ya Ajira na Mahusiano Kazini na pia kuagiza wafanyakazi wote warudishiwe fedha walizokatwa kinyume na sheria katika mshahara wao kwa ajili ya kununua vifaa kinga na kuwataka waajiri wasikwepe jukumu la kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa afya na usalama wao wakiwa kazini.

Akiwa wilayani  hapo Naibu Waziri Mavunde amepata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya HISOON Ltd kutoka China James Lee ambaye amevutiwa na sera na mazingira ya uwekezaji nchini na sasa anakamilisha taratibu za uwekezaji mkubwa wa kiwanda kikubwa cha Makaratasi ambacho kitakuwa uwezo wa kuzalisha tani laki tano za karatasi na ambacho pia kinatarajiwa kuajiri wafanyakazi wasiopungua 5000.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,  Vijana, Kazi na Ajira, Mhe Anthony Mavunde akizungumza na viongozi na watumishi wa kiwanda cha Hong Wei kilichopo wilayani Mufindi mkoani Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...