UVUVI haramu wa kutumia mabomu umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na takwimu kuonesha ndani ya mwaka wa 2019 hakuna tukio lolote lililojitokeza la uvuvi wa kutumia mabomu.

Hayo yamesemwa  leo na  Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo  Abdallah Ulega baada ya kutembelea Mnada wa uuzaji Samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mnada huo  Waziri Ulega amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Serikali na wavuvi ndo chanzo cha kutokomeza uvuvi wa kutumia mabomu hapa nchini.

"Hakuna mlipuko wa mabomu kwasasa hivyo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kuna watu wamebaki vilema kwaajili ya hayo mabomu, ninyi mnatakiwa mtuunge mkono kuhakikisha msirudi nyuma, serikali ya awamu ya tano ipo kwaajili ya kushirikiana na wananchi wake". Amesema Waziri .Ulega.

Pamoja na hayo  Ulega amewataka wavuvi kuwa kila mtu kuwa mlinzi wa mwingine ili kuhakikisha kila mmoja anafuata utaratibu na sheria zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu.

Aidha,  Ulega amesema kuwa suala la wavuvi kutumia nyavu za kisasa maarufu kama Ringnet wakati wa mchana amesema serikali italifanyia kazi katika kipindi hiki ambacho wanafanya uboreshaji wa kanuni  za uvuvi

Amesema lengo ni kuboresha mazingira katika sekta ya uvuvi na kuhakikisha mazingira ya bahari yanahifadhiwa pamoja na kutoathiri upatikanaji wa dagaa ambao ni biashara kubwa kwa wavuvi hao  na wakina mama ambao hufika hapo na kununua kwenda kuuza na kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji yao.

kuhusu leseni,  Ulega amewatoa wasiwasi kwamba mvuvi hapaswi kuwa na leseni zaidi ya moja na kwamba mvuvi anapokuwa na leseni moja inamtosha kuendesha shughuli  za uvuvi mahali popote

"Leseni ya uvuvi ni moja ukikata Mkuranga utatamba nayo mpaka Mtwara, ukikata Mtwara utatamba nayo mpaka Lindi mpaka Tanga".Amesema Ulega.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Daniel Chongolo amewaahidi wavuvi wa eneo hilo kushughulikia suala la ujenzi wa choo ambao utakamilika kufikia mwezi Disemba mwaka huu utakua umemalizika ujenzi huo.
Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na wavuvi pamoja na wananchi  waliofika katika eneo la mnada wa Samaki Kunduchi wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaomba Wavuvi hao  kufanya kazi  bila kuwa na wasiwasi  kwa kufuata sheria  kanuni  na taratibu.

Wavuvi  pamoja na wananchi wa maeneo mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega baada ya kutembelea mnada wa  Samaki Kunduchi wilaya ya Kinodoni  Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (kushoto) akizungumza wavuvi  pamoja na wachuuzi wa samaki katika eneo la mnada  wa samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam ambapo ameahidi kuboresha miundombinu mbalimbali katika mnada huo,Kulia ni Naibu Waziri wa Uvuvi, Mh.Abdallah Ulega wa pili kulia ni Diwani wa kata ya Kunduchi,Michael Urio

  Diwani wa kata ya Kunduchi   wilaya ya Kinondini Jijini Dar es Salaam,Michael Urio akimshuru  Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega kwa kufika endeo la mnada wa samaki Kunduchi na kufanya mkutano wa kusikiliza kero za wavuvi.
 Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa  maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam waliofika katika eneo mnada wa wa Samaki Kunduchi leo.
 Mwenyekiti wa B.M.U Kunduchi wilaya ya Kinondoni jiji Dar es Slaam,Zedi Mwinyi wa kwanza kushoto akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega namana kazi zinavyo fanyika katika mnada wa kuuzia Samaki.
  Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwasili katika mnada wa kuuzia Samaki wa Kunduchi wilaya ya Kinondino jijini Dar es Salaam.

 Mkutano ukiendelea 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...