JESHI la polisi mkoani Pwani, limekamata watu Tisa wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya utapeli kwa kutumia simu za mkononi na laini za simu kutoka makampuni mbalimbali na orodha ya namba za simu za watu .

Watu hao ,walikuwa wakituma ujumbe mfupi sms,kwamba watumiwe pesa na kujifanya waganga wa jadi wanazindika,kusafisha nyota za watu, ndoa na biashara.

Akithibitisha kuhusiana na tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alieleza, agost 13 mwaka huu,kata ya Zinga na Yombo wilayani Bagamoyo,walikamatwa watuhumiwa hao wakiwa na simu za mkononi 14,laini za simu za makampuni mbalimbali 22 na orodha ya namba ya simu za watu 16 zilizoorodheshwa kwenye karatasi.

Aliwataja majina yao kuwa ni, Suleimani Athuman (35), Hamis Iddi (30), Dipinde Pango,Adam Nestory,Hamis Kondo,Deus Swai , Julius Joseph(27) na Mohammed Bruno (33) .

Wankyo alibainisha kuwa ,watuhumiwa hao wanahojiwa ni namna gani wanafanya uhalifu wao kwa kutumia mtandao ya simu na kufanya wizi wa pesa kwa kuchepusha salio la pesa ya mtu kwa makusudi ya uhalifu.

"Watafikishwa mahakamani baada ya mahojiano na uchunguzi kukamilika"alifafanua kamanda huyo.

Wankyo aliitaka jamii kufanya shughuli halali za kujiongezea kipato badala ya kufanya uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...