Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa anatarajiwa kuongoza kongamano la majadiliano kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Wananchi Kusini mwa Afrika(SADC).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbasi amesema kupitia kongamano hilo mzee Mkapa atatoa uzoefu na uzeefu wake kuhusu nchi za SADC.

Dk.Abbasi amefafanua pamoja na mambo mengine, kuna ratiba ya shughuli mbalimbali kuhusu SADC , Agosti 15 mwaka huu Mkapa atakuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako ndiko kongamano hilo litafanyika. 

"Kwenye kongamano ambalo litafanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutakuwa na majadiliano kuhusu nchi za SADC.Mzee Mkapa siku hiyo ataongoza majadiliano hayo kwa kutoa uzoefu na kama tunavyofahamu amekuwa kiongozi wetu kwa muda mrefu,anao uzoefu mkubwa kuhusu SADC ,hivyo tutajifunza mengi kutoka kwake,"amesema Dk.Abbas.

Amesema ni vema wananchi wakajitokeza kwenye kongamano hilo kwani wanaamini litakuwa na somo kubwa kuhusu nchi za jumuiya hiyo ambayo Tanzania imebeba historia kubwa kutokana na mchango wake ,kwanza wa kukomboa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika lakini sasa ni katika kushirikiana katika kuleta maendeleo kwa nchi wanachama na Afrika kwa ujumla.

Wakati huo huo Dk.Abassi ametoa ufafanuzi kuhusu uwepo wa tetesi kuwa baadhi ya washiriki wachache wameshindwa kushiriki kwasababu mbalimbali ikiwemo ya kukwama mikakati.

Katika hilo Dk.Abass ameeleza madai hayo hapana ukweli na kwa kuwa ni fununu ni vema zikaachwa lakini akatumia nafasi hiyo kueleza nchi zote za jumuiya hiyo nimepata nafasi ya kushiriki na taratibu za kushiriki zinaeleweka. " Hizi ni fununu tu ambazo hazina uthibitisho.Na kwa kuwa fununu tuaache.

"Binafsi nimepita kwenye banda Leo,nimeona namna ambavyo mabanda mengi yalivyokuwa na bidhaa nzuri,tuendelee kuwahamaisha wananchi kuja kutembelea na hakuna kiingilio,"amesema Dk.Abbassi na kuongeza mbali ya kuwepo na mabanda kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere pia viwanj vya Karimjee nako kuna mabanda ya biashara na kote huko amehamasisha wananchi kwenda kutembelea na kuona bidhaa.  
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi akifafanua jambo na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya wiki ya nne ya viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Picha na Michuzi Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...