RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia Meli Mpya ya Mafuta ya MT.UKOMBO II,Ikiwasili kuelekea katika bandari ya Malindi Zanzibar ikitokea Shanghai Nchini China, iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyard ya Uholanzi.(Picha na Ikulu) 
……………. 

HATIMAE ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyowaahidi wananachi wa Zanzibar kuwa Serikali anayoiongoza itanunua meli mpya ya mafuta MT MKOMBOZI II leo imetimia baada ya meli hiyo kuwasili katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Shanghai nchini China. 

Rais Dk. Shein akiwa Ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar alipata fursa ya kuiona meli ya MT MKOMBOZI II ikiwasili kutoka ukingoni mwa pwani ya Zanzibar ikitokea usawa wa kisiwa cha Chumbe na kuelekea katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja ilipokwenda kutia nanga. 

Akiwa katika varanda ya jengo la Ikulu mjini Zanzibar Rais Dk. Shein alionekana akiwa na furaha kubwa wakati akiiangalia meli hiyo ikiwasili ikiwa ni kutokana na ahadi aliyoitoa na azma yake juu ya ujio wa meli hiyo mpya ya mafuta. 

Meli hiyo iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyard ya nchini Uholanzi iliwasili rasmi katika Bandari ya Malindi Zanzibar majira ya saa saa tano za asubuhi na kupata mapokezi ya aina yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...