Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa kwenye chanzo cha maji cha Bukanga kinachotumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), mkoani Mara. 
Magari mawili ya majitaka ya Mradi wa Majitaka wa Manispaa ya Musoma Mjini unaotekelezwa na Kampuni ya Lahmeyer GKW Consult, mkoani Mara 

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua moja ya magari mawili ya majitaka ya Mradi wa Majitaka wa Manispaa ya Musoma Mjini unaotekelezwa na Kampuni ya Lahmeyer GKW Consult, mkoani Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na viongozi na wataalam wa mkoa wa Mara, pamoja na wataalam wa Kampuni ya Lahmeyer GKW wanaotekeleza ujenzi wa Mradi wa Majitaka Musoma mjini, mkoani Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiangalia ujazo wa maji kwenye tenki la maji la Nyamiongo lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 5, katika Manispaa ya Mji wa Musoma, mkoani Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akipokea maelekezo ya ujenzi wa Mradi wa Majitaka katika Manispaa ya Mji wa Musoma kutoka kwa Mhandisi Mshauri Mkuu, Rweyemamu Kassimbi, mkoani Mara. 
………………… 
Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa Saudia (SFD) zipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mugango-Kiabakari katika mkoa wa Mara. 

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametoa kauli hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi katika kufuatilia na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa mkoani Mara. 

Amesema mkataba huo utakaogharimu Dola za Marekani milioni 30.69 unatarajiwa kusainiwa tarehe 15 Agosti, 2019 unalenga kuboresha huduma ya maji katika maeneo ya Mugango, Kiabakari na Butiama, na kwa sasa hatua ya usanifu wa kina na uandaaji wa makabrasha ya zabuni umekamilika na taratibu za kumpata Mkandarasi zinaendelea. 

Kazi ya uboreshaji ya mradi huo mkongwe ulioanza mwaka 1974 itakapokamilika utanufaisha wananchi wapatao 80,000 waliopo katika eneo la mradi pamoja na vijiji 13 vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka bomba kuu. Serikali imetenga Shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo. 

Wakati huo huo, Naibu Waziri Aweso amesema Mtaalam Mshauri kutoka Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India tayari ameanza kazi ya upembuzi yakinifu kwa miradi ya maji katika miji ya Rorya, Tarime na Mugumu mkoani Mara tangu tarehe 1 Juni, 2019 na atakamilisha kazi hiyo ifikapo tarehe 31 Agosti, 2019. 

Akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kumaliza tatizo la maji katika maeneo yote yaliyo pembezoni mwa Ziwa Victoria. 

Miji ya Rorya, Tarime na Mugumu ni miongoni miji itakayonufaika na Mradi wa Maji wa Miji Mikuu ya Wilaya 29 inayotekelezwa na Serikali kwa kutumia mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kupitia Benki ya Exim ya India.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...