Baadhi ya wanachama wa federation wakichangia damu katika hospital ya taifa Muhimbili kitengo cha damu salama.
Mratibu wa taasisi ya family Federation Bw. Semeni Kingaru aliyefanikisha shughuli nzima ya uchangiaji damu 
Muuguzi  Mwandamizi katika Hospital ya  Taifa Muhimbili kitengo cha damu Judith Mayombo akizungumza jambo na baadhi Wadau waliojitokeza kujitolea damu 

*****************

Na Stahmil Mohamed

Taasisi ya family Federation for  World peace imeahidi kumaliza upungufu wa damu nchini kwa kuendesha zoezi la uchangiaji damu kila mwisho wa wiki ili kuokoa watu mbalimbali wenye uhitaji wa damu.

Akizungumza kwa niaba ya kiongozi wa Taifa wa shirikisho hilo wakati wa uchangiaji damu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Bw Semeni Kingaru ambaye ni mratibu wa masuala mbalimbali ya taasisi hiyo amesema kuwa kutokana na uhaba wa damu uliopo nchini taasisi hiyo ambayo inawanachama zaidi ya elfu 80 wameanzisha utaratibu wa uchangiaji damu kila mwisho wa juma.

"Lengo hasa ni kupunguza changamoto hiyo pia kuokoa maisha ya watu mbalimbali wenye uhitaji Wa damu wakiwemo majeruhi wa ajali, wanawake wajawazito wanaokwenda kujifungua hata watoto wenye uhitaji wa damu",alisema Kingaru

Imesema kutokana na hamasa waliyonayo wanachama wa taasisi hiyo katika suala la uchangiaji damu,wanaamini kuwa uhaba wa damu utapungua na watu mbalimbali wataweza kuokoa maisha kama ilivyo kauli mbiu yao ya 'ishi kwa ajili ya wengine' .

Wanachama wa family Federation Irene na Nasibu Mbarook  waliojitokeza kuchangia damu katika hospital ya Taifa ya Muhimbili ,wamesema kuwa wameamua kuchangia damu katika hospital hiyo Kwani wanajua uhaba wa damu uliopo katika hospital hiyo ya Taifa, Kwani kuna watu mbalimbali wenye uhitaji wakiwemo majeruhi wa ajali.

Kwa upande wake Judith Mtayombo ambae ni Muuguzi mwandamizi katika kitengo cha damu Hospital ya Taifa Muhimbili amewaomba Watanzania kujijengea utaratibu wa kuchangia damu ili iweze kusaidia Wagonjwa mbalimbali waliopo wodini pia inapotokea majanga makubwa kusiwepo na changamoto ya upatikanaji wa damu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...