Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, baada ya mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, baada ya mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Benki na Serikali ya Tanzania.
Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (kulia) na Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara hiyo, Bw. Shogholo Msangi, wakifuatilia mazungumzo kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na Serikali ya Tanzania
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagamba (wa pili kushoto), akieleza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), Jijini Dar es Salaam. (Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam


Uhusiano wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania umeimarika baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia nchi 22 zilizoko Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa Benki hiyo iko tayari kutoa kwa Tanzania fedha zote za mkopo wa masharti nafuu kiasi cha dola za marekani bilioni 1.7 zilizobaki katika mgao wa 18 wa IDA.

Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutolewa kabla ya kuanza mgao mpya wa 19 wa IDA utakaoanza Julai 2020, baada ya kukamilisha taratibu zote za upatikanaji wa fedha hizo.

”Fedha hizi zitaelekezwa katika kutekeleza miradi kadhaa muhimu ikiwemo ya Elimu, Afya, Mradi wa kusaidia Kaya Masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF, Awamu ya Pili na Uendelezaji wa Miji na Masuala ya Uchumi Jumuishi Visiwani Zanzibar” alisema Bi. Kabagambe

Aidha, alipongeza hatua kubwa zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli, katika kupiga vita rushwa na ufisadi nchini pamoja na kutekeleza miradi ya jamii kwa umahili mkubwa ikiwemo miradi ya kimkakati ya reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa pamoja na mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya maji katika mto Rufiji wa Julius Nyerere.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameiomba Benki hiyo kuisaidia Serikali kwa kuipatia fedha za kufanikisha ujenzi wa miundombinu hiyo ya umeme, reli, maji safi na salama, kuimarisha sekta ya kilimo, viwanda, bandari, rasilimali watu na masuala ya teknolojia ya habari na Mawasiliano-TEHAMA.

Alibainisha kuwa miradi hiyo itachochea zaidi ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini wa wananchi kwa kuwa nishati ya umeme itachochea ukuaji wa sekta ya viwanda hivyo na kukuza ajira, wakati reli imara na ya kisasa itaimarisha mtandao wa reli na kuwa uti wa mgongo wa maendeleo ya Tanzania na nchi za Ukanda wa Afrika kwa ujumla.

Amepongeza pia uamuzi wa Benki hiyo wa kuruhusu upatikanaji wa fedha kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.7 na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika sekta ya elimu, kusaidia kaya maskini kupitia TASAF, kuendeleza masuala ya uchumi jumuishi Visiwani Zanzibar, masuala ya ardhi na miundombinu ya barabara ili kuboresha shughuli za kiuchumi katika jamii.

Akitoa majumuisho ya mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na Mgeni wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa Serikali inapongeza uamuzi wa Benki wa kuendelea kuipatia fedha serikali ya Tanzania kwa manufaa ya wananchi.

Mpaka sasa, Benki ya Dunia imefadhili miradi 28 ya Maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.0 sawa na takriban sh. trilioni 11.5, ambapo miradi 20 ni ya kitaifa yenye thamani ya dola 4.065 bilioni na miradi 8 ni ya kikanda yenye jumla ya dola za Marekani 938 milioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...