Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu

TANZANIA ambayo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) imetaja mambo matatu muhimu ambayo itayapa kipaumbele katika kuyatekeleza ndani ya jumuiya hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wakati anazungumza na waandishi wa habari leo Agosti 21,2019 jijini Dar es Salaam.

Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine lakini ni vema wakaeleza mambo muhimu matatu yatakayopewa kipaumbele.Amesema jambo la kwanza ni kuhakikisha lugha ya Kiswahili inazungumzwa kwenye nchi za jumuiya hiyo na hiyo ni baada ya wakuu wa nchi hizo kuipitisha rasmi kuwa lugha ya nne ya jumuiya hiyo.

Akifafanua zaidi kuhusu Kiswahili, Profesa Kabudi amesema haikuwa kazi rahisi kukipigania Kiswahili kuwa rasmi kwenye nchi hizo na kwamba mkakati wake ulianza Machi mwaka huu.

"Mkakati wa kukipigania Kiswahili ni baada ya majadiliano ya muda mrefu kwenye kikao cha mawaziri wa nchi wanachama wa SADC, hatimaye Mwenyekiti wa Jumuiya alitoa ombi kwa wakuu wa nchi na hatimaye imepitishwa.

"Ni jukumu letu Watanzania kuhakikisha tunachangamkia fursa hiyo ikiwemo ya kufundisha Kiswahili.Kwa sasa nchi za Kenya na Congo wananufaika sana na lugha hii maana wengi wao wamekuwa walimu wa Kiswahili kwenye mataifa mengine.Nasi tuna kila sababu ya kutumia fursa hii,"amesema.

Ameongeza ni vema watanzania wakajifunza lugha za kigeni ikiwemo Kifaransa na Kireno kwani hiyo itapaua wigo zaidi maana utakuwa unajua Kiswahili na wakati huo huo unafahamu na lugha nyingine.Waziri Kabudi amesema jambo la pili ambalo litapewa umuhimu ni kuhakikisha mkakati wa viwanda kwa nchi wanachama unatekelezwa kama ambavyo wamekubaliana wakuu wa nchi hizo.

Amesema ambacho kitafanyika ni kuwepo kwa mpango mkakati kwa kila nchi kufanikisha uwepo wa viwanda kwa maendeo ya nchi hizo.Amefafanua ni matarajio yao kuona kunakuwa na kiwanda au viwanda vya mfano kwa nchi za SADC huku akifafanua namna ambavyo Serikali ya Tanzania imejipanga kikamilifu kwenye eneo hilo.

"Tanzania tumepiga hatua sana katika viwanda , na hata kwenye maonesho ya bidhaa kwa nchi za SADC bidhaa zetu zimekuwa kivutio kutokana na ubora wa bidhaa zetu.Waliotembelea viwanda vyetu wamethibitisha na kufurahishwa na teknolojia ya hali ya juu katika utengenezaji bidhaa,"amesema.

Wakati jambo la tatu ambalo watalipa kipaumbele ni kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo zinasimama kidete katika kushinikiza jumuiya ya kimataifa kuoindolea vikwazo nchi ya Zambabwe.Amesema na katika kutekeleza hilo wamekubaliana nchi zote za SADC Oktoba 25,2019 iwe ni siku ambayo kutakuwa na shughuli au mijadala kwa kila nchi inayozungumzia Zimbabwe kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.

Waziri Kabudi amesema hakuna sababu ya nchi hiyo kuendelea kuwa na kuwekewa vikwazo wakati wananchi wamefanya uchaguzi na kupata Rais wao kwa uhuru na kusisitiza kuendelea kuiwekea vikwazo nchi hiyo ni kuendelea kuwatesa wananchi.

"Kama kulikuwa na sababu za nchi hiyo kuwekewa vikwazo kwa sasa tunaamini havipo tena.Jumuiya ya Kimataifa itoe vikwazo kwa Zimbabwe.Tumekubaliana katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mwaka huu tutakwenda na ajenda hii, lazima Zimbabwe iondolewe vikwazo na kwa kuwa Tanzania ndio Mwenyekiti wa SADC tumedhamiria katika hili,"amesema Waziri Kabudi.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na Wakuu na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akifafanua jambo kwa msisitizo mbele ya Wakuu na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar, 
 Baadhi ya Wahariri wakuu wa Vyombo vya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Kabudi .
Mmoja wa Wanahabari akiuliza swali kwa Waziri Kabudi
 Baadhi ya Wahariri wakuu wa Vyombo vya habari  na Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Kabudi . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...