SHIRIKA la viwango Tanzania limepanga kufanya msako kwenye viwanda vyote za kuzalisha nondo nchini ili kujiridhisha kama nondo zinazozalishwa zinazikidhi viwango vya ubora wa nondo.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi huo uliofanywa kwenye maeneo ya Kawe, Buguruni, Mwenge na Tegeta mwishino juzi, Mkaguzi wa TBS, Mhandisi Donard Manyama,  alisema katika ukaguzi wao wamebaini kuwepo kwa nondo nyingi zisizokidhi viwango kwenye matumizi ya ujenzi.

"Ukaguzi wetu umebaini kuwepo udanganyifu katika uzalishaji wa nondo kuanzia unene, urefu na madaraja vyote hivyo hakuna ukweli jambo hili ni hatari kama litafumbiwa macho," alisema Mhandisi Manyama

Alisema kiwango halisi cha urefu wa nondo huwa ni ujazo husiopungua futi 40, lakini zilizopo sokoni baadhi zina futi 39 hadi 34, huku unene yaani ujazo wa kipenyo halisi ni  mm 18, lakini zilizopo sokoni nyingi ni ujazo 9 hadi 6.
 
Alizungumzia pia kuhusu udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara kuuza bei moja kati ya nondo za daraja la BS 300 na 500, Mhandisi Manyama alisema kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kwa upande wake Mhandisi Nyabuchweza Methusel alisema ukaguzi huu umetoa matokeo hasi ambayo TBS wanaona kama changamoto kwao na kwamba  yasipodhibitiwa mapema yanaweza kuzalisha majanga ya hatari kwa majengo kuporomoka.

Mhandisi Methusel alisema hatua hiyo italazimu kila mzalishaji wa nondo kuanza kutekeleza matakwa ya sheria ya viwango ambayo inamtaka kila mzalishaji kuweka jina la kampunii, ujazo na urefu kwa kila nondo inayozalishwa.

Mmoja wa mafundi ujenzi, Patrick Jacob, alipongeza hatua kazi kubwa inayofanywa na shirika hilo kuhakikisha nondo ambazo hazikidhi viwango zinaondolewa kwenye soko hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...