*Vijana wapata fursa ya kujifunza na kujiajiri wenyewe, waushukuru ubalozi wa China nchini

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BARAZA la michezo nchini (BMT) kwa kushirikiana na chama cha Wushu pamoja na vituo vya lugha ya kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam wameendesha mashindano ya kimataifa ya sita ya Wushu jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha washiriki 200 kutoka nchini Tanzania na washiriki 20 kutoka nchini Rwanda.

Akizungumza mara baada ya mashindano hayo  mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambaye ni mwakilishi wa katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa (BMT) Milinde Mahona amesema kuwa ubalozi wa China nchini umekuwa ukifanya jitihada za ziada katika michezo na chama cha Wushu kipo kwenye orodha ya vyama vinavyofanya vizuri na hiyo ni kutokana na uongozi bora na ameupongeza ubalozi wa China nchini kwa ushirikiano wanaoonesha kwa vijana hao.

Amesema kuwa ubalozi wa China nchini umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha na kushirikiana na  vijana katika suala la kujiajiri kupitia michezo na kusema kuwa ubalozi umekuwa ukileta walimu kutoka China ili kuwafundisha vijana hao.

Milinde amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kusaidia chama hicho ambacho hadi sasa wameanzisha chama chao cha ulinzi pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi na kuwashauri  viongozi wa chama hicho kupeleka mafunzo hayo mikoani ili waweze kuwafikia vijana wengi zaidi.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa China nchini Gao Wei amesema kuwa mashindano hayo yataendelea kila mwaka kwa kushirikisha nchi mbalimbali Afrika Mashariki kama yanavyofanyika nchini China.

Gao amesema kuwa maarifa ya Wushu yaliyotolewa nchini yanaweza kuwa hazina kwa kutoa mafunzo kwa nchi nyingine, na amewashauri vijana hao kuendelea kuzalisha miradi mingi zaidi ambayo inatoa ajira kwa vijana wengi zaidi.

Vilevile ameeleza kuwa michezo hiyo imelenga kukuza nidhamu ambapo wizara inayosimamia masuala hayo imeona umuhimu mkubwa wa kituo hicho na wao wataendelea kuwaunganisha vijana kutoka sehemu mbalimbali kupitia Wushu.

Mashindano hayo yalizikutanisha timu nane kutoka Tanzania bara kwa kuhusisha Mikoa mbalimbali nchini pamoja na timu ya Rwanda Kungfu Wushu Federation ya nchini Rwanda.
 Viongozi mbalimbali waliohudhuria mashindano hayo ya sita ya Wushu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha vijana kutoka Tanzania na Rwanda, ambapo wito umetolewa kuwa chama hicho Cha Wushu kipelekwe Mikoani ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika, leo jijini Dar es Salaam.
 Vijana wa Wushu kutoka Mikoa mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Rais wa Wushu nchini Salehe Muhindi akizungumza katika hafla hiyo ambapo ameushukuru ubalozi wa China nchini kwa ushirikiano na kuahidi kuendelea kuunganisha vijana kote barani Afrika kupitia Wushu, leo jijini Dar es Salaam.
Washindi wa Wushu msimu wa 6 wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...