Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation (VTF) leo imesaini mkataba wa makubaliano na WWF (World Wide Fund for Nature) ili kuchangia milioni 303 kwa ajili ya mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya makamu wa rais kwa kushirikiana na WWF. Hafla hiyo ya usainishaji ilifanyika leo katika ofisi za WWF jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dr Thomas Bwana aliyemwakilisha Mgeni rasmi naibu katibu mkuu katika Wizara hiyo Mheshimiwa Balozi Joseph Sokoine.. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dr Bwana amesifu mpango wa Vodacom Tanzania Foundation na WWF (World Wide Fund for Nature) kupambana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi. Pia aliongeza kuwa amefurahi namna makampuni na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanavyoungana kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu namba 13 juu ya hali ya hewa. 

“Kutokana na asilimia 80 ya watu kutegemea mazingira na maliasili kwa ajili ya kutengeneza kipato, kulinda maliasili ni jambo muhimu litakalochochea mafanikio ya kufikia mpango wa maendeleo ya kiuchumi. Serikali imeweka mikakati kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi nchini Tanzania pamoja na kuhakikisha kuwa jamii inamifumo ya kukabiliana na mabadiliko haya, jambo linalofanya tufurahie ushirikiano huu.” 

Aidha Dk Bwana aliongeza kuwa serikali ina mpango wa kupanda miti milioni 280 kila mwaka ili kuunga mkono mpango wa taifa wa kusimamia na kupanda miti kwa ajili kuifanya nchi yetu kuwa ya kijani. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia, amesema kuwa wamefurahia kuingia ubia na WWF ili kutekeleza mpango huo ambao unawiana na mpango mkakati wa VTF kwa mwaka 2019/21 ambao umejikita katika kuchochea hatua za kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi. 

Kama kampuni ya Vodacom, maono yetu ni kuwaunganisha watu ili kuleta maendeleo Tanzania, tuna matumaini ya kuunda jamii ya kidijitali, tukilenga kujenga uchumi jumuishi na kufanya kazi katika sayari ambayo athari zetu ni ndogo. Mradi huu umejidhatiti katika kuifanya Dodoma kuwa ya kijani lakini tunatumaini uwepo wa ongezeko la hatua za kisasa dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka ufahamu na uhamasishaji wa jamii,” alisema Mworia. 

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru amesema kuwa mfuko huo utaelekezwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti 100,000 kwa mwaka wa kwanza na kutengeneza bustani ndani ya mji mkuu pamoja na kuongeza ufahamu na kuhamasisha jamii kwa kuwapa mafunzo makundi ya vijana na wanawake katika uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki mbadala na kusimamia taka kama shughuli ya kuwawezesha kiuchumi. 

Tumejidhatiti kuunda miradi endelevu ambayo itasaidia kudhibiti changamoto za kimazingira na kijamii nchini Tanzania. Tunaishukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa kutuunga mkono katika kutekeleza mpango huu. Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaonekana katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo kurejesha mfumo wa ikolojia na kulinda maliasili ni njia mahususi ya kuzuia madhara yenye uwezo wa kuharibu maisha ya watu na utekelezaji wa mradi huu utakuwa ni hatua kubwa sana katika kushughulikia changamoto hizo,” aliongeza Dr Ngusaru. 

Mradi huo uliopewa jina “kuishi kwa amani na mazingira asili” utaanza rasmi mwezi Septemba mwaka huu na utatekelezwa kwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa rais – mazingira, halmashauri ya jiji la Dodoma na taasisi ya huduma za misitu (TSF).




Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (kulia) pamoja na Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru (kushoto) wakisaini makubaliano yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 303 milioni kwa ajili ya mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF. Wanaoshuhudia ni Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Thomas Bwana (katikati), Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kulia) na Meneja Washirika na Maendeleo wa WWF Dk Severine Kalonga. Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imedhamiria kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha mazingira endelevu (sustainable environment) pamoja na maendeleo.



Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (kulia) akibadilishana mkataba na Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru (kushoto) ambao una thamani ya Shilingi za Kitanzania 303 milioni kwa ajili ya mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF. Anayeshuhudia ni Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Thomas Bwana. Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imedhamiria kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha mazingira endelevu (sustainable environment) pamoja na maendeleo.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 303 milioni, Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru (kushoto), kwa ajili ya kudhmaini mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF. Anayeshuhudia ni Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Thomas Bwana (katikati). Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imedhamiria kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha mazingira endelevu (sustainable enviroment) pamoja na maendeleo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...