Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (kulia) akimkabishi Rais wa
shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia (Kusho ),
mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 9, fedha
ambazo zimetolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania kudhamini ligi
kuuTanzania bara kwa kipindi cha miaka mitatu (2019/2021), katika hafla
fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es
Salaam jana. Anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe,
akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza udhamini
wa ligi kuu ya Vodacom iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini
Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom imetoa kiasi cha sh. bilioni 9
kudhamini ligi kuu ya Tanzania bara kwa kipindi cha miaka mitatu
(2019/2021) kwa lengo la kuinua vijana wenye vipaji vya mpira wa miguu
nchini na kuchochea maendeleo kwa ujumla. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hisham Hendi na Kulia ni Rais wa
shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hisham Hendi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya udhamini uliotolewa na kampuni Vodacom kwenda TFF kwa ajili ya Ligi kuu ya Tanzania Bara, katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kampuni ya Vodacom imetoa kiasi cha sh bilioni 9 kudhamini ligi kuu Tanzania bara kwa kipindi cha miaka mitatu (2019/2021) kwa lengo la kuinua vijana wenye vipaji mpira nchini na kuchochea mendeleo kwa ujumla. Kulia ni Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia
Vodacom Tanzania kudhamini ligi kuu ya Tanzania kwa miaka mitatu
Agosti 23, 2019 – Dar es Salaam: Ligi kuu ya Tanzania yarudi kwa kishindo baada ya
Vodacom Tanzania na shirikisho la soka TFF kufikia maridhiano na Vodacom
kudhamini ligi hyo. Kampuni hiyo imesaini mkataba na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ambao utawezesha shirikisho hilo la soka kupokea TZS bilioni
9 za udhamini kwa kipindi cha miaka mitatu (2019/2021), na kupelekea Vodacom
kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo.
Ushirikiano na udhamini huo
ulitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya Vodacom,
jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, na umehusisha pande zote ambazo ni
kampuni ya Vodacom Tanzania, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
bodi ya ligi.
Ligi kuu ya Tanzania ambayo sasa itaitwa Ligi kuu
ya Vodacom itaanza tarehe 24 ya mwezi huu, ikitarajia kushuhudia jumla ya
michezo 380 ikichezwa katika viwanja
mbalimbali nchini na kushirikisha timu 20 zilizoko ligi kuu ya Tanzania bara.
Akizungumza katika hafla hiyo Dk
Mwakyembe alisema serikali imepiga hatua kubwa katika kuwezesha vijana wenye
vipaji mbali mbali nchini na alisisitiza umuhimi wa kuwekeza katika Vijana ili
kuleta Maendeleo nchini. Pia aliipongeza Vodacom kwa kutia chachu juhudi za
serikali katika kufanikisha malengo hayo.
“Ukweli ni kwamba tupo katika wakati ambao
tunahitaji kushirikiana na vijana katika kuleta maendeleo ya kijamii na
kiuchumi, ambapo mpira wa miguu unaajiri mamia ya vijana hao. Uwekezaji
uliofanywa na Vodaom siku hii ya leo ni moja ya ngao ya kuleta mabadiliko
makubwa katika mpira wamiguu nchini, vile vile kuongeza ajira kwa vijana.
Napenda kuwasihi wawekezaji kuwekeza katika michezo mbali mbali ili kufanya
vijana wetu wawe wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya uchumi,” aliongeza
Mwakyembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom
Bwana Hisham
Hendi amesema kuwa kampuni ya Vodacom iko mstari wa mbele
katika kuunga mkono maendeleo na shughuli za mpira wa mguu hapa inchini hivyo
leo ni siku ya furaha sana kwao.
“Tumedhamini
ligi hii kwa zaidi ya miaka 9 na tumeona vipaji vingi vikiibuka na ligi
kuongezeka umaarufu nchini na nje ya nchi ikufuatiliwa na mamilioni ya
washabiki. Wote tumekubali kuwa wanamichezo ni mabalozi wazuri wa nchi yetu
kama tulivyoona katika michuano ya AFCON iliyoisha hivi karibuni. Ni wajibu
wetu kuhakikisha kuwa tunawaunga mkono katika kutambua na kukuza vipaji vyao
kadri tutakavyo weza” alisema Hisham .
Bwana Hendi aliongeza kuwa amejivunia kampuni hiyo
kurejea kuidhamini ligi kuu kwa kipindi kingine na kufafanua kuwa itaendelea
kuwa mdau wa kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo hapa Tanzania.
Pia aliweka wazi kwamba ligi kuu ya
Vodacom inakuja na ofa kabambe kwa wateja wao pamoja na mashabiki wa mpira
kupitia huduma ya SOKA LETU. “Pale mteja anapojiunga na SOKA LETU anapata
dondoo mbali mbali za michezo, ikiwemo VPL na si hayo tu, sasa anapata nafasi
ya kujishindia dakika au tiketi ya kwenda kutizama michuano itakayokuwa
ikiendelea na zawadi nyingie kabambe,” alisisitiza Hendi.
Kwa upande wake Rais wa TFF, Wallace Karia,
ameipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania akisema kuwa anaamini, maendeleo ya sasa
yatalenga zaidi katika kuunga mkono vipaji vipya na vilivyopo ndani ya
nchi. “Kwa niaba ya TFF, napenda kuwashukuru Vodacom Tanzania kwa
kuonyesha nia na kuendelea kuunga mkono mpira wa miguu nchini. Nasi tunaahidi
kuendelea kuthamini vipaji vya wachezaji wetu na kuhakikisha tunapata mafanikio
zaidi,” alisema Karia.
“Ikiwa ni sehemu ya malengo yetu ya kuipeleka
Tanzania katiza zama na malipo kwa njia ya kidigitali, Sasa wateja wetu wote na
mashabiki wa mpira watanuua tiketi zao kupitia M-Pesa kutoka mtandao wowote
hata mabenki. Kwa kweli ukiwa na Vodacom yajayo yanafurahisha,” alihitimisha Bw
Hendi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...