Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania Noel Mazoya, alipotembelea banda lao katika maonyesho ya nne ya Viwanda ya Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC), yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom Tanzania ni miongoni mwa wadhamini wa maonyesho hayo, ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika. Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania Jacqueline Materu
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya akisoma ripoti ya uwekezaji katika maendeleo ya watu na mpango mpya ya Vodacom Tanzania Foundation, aliyenaye ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Alex Bitekeye, katika banda lao kwenye mkutano wa 39 wa SADC , jijini Dar es salaam, hivi karibuni. Katika mkutano huo kampuni ya Vodacom Tanzania imedhamini upande wa mawasiliano ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya akisikiliza huduma mbali mbali zitolewazo na kampuni ya Vodacom Tanzania kutoka kwa Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo, Alex Bitekeye, katika banda lao kwenye mkutano wa 39 wa SADC , jijini Dar es salaam, hivi karibuni. Katika mkutano huo kampuni ya Vodacom Tanzania imedhamini upande wa mawasiliano ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...