Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

SERIKALI imesema kuwa walimu wa somo la Fizikia ni bado ni wachache na kutaka vyuo vya ualimu kuandaa walimu hao ili  kwenda sambamba na malengo ya serikali.

Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolijia Dkt. Evamaria Semakafu wakati wa kufunga mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu  jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa walimu wa hisabati na Kemia kwa sasa hakuna upungufu mkubwa bali  changamoto ni walimu wa somo la Fizikia.

Amesema kuwa serikali inatekeleza mikakati mbalimbali  kuhakikisha elimu ya ualimu inatolewa kwa  viwango na kulingana  na sasa ya kitaifa huku  nafasi ya wadau ikipewa kipaumbele.

Dkt.Semakafu anasema kuwa nia ya Serikali ni kuhahakikisha vyuo vinaandaa wali wenue umahiri ,weledi na ubunifu katika ufundishaji.

Aidha ameitaka Wakala wa  Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ,(Adem) kusamama katika kutekeleza jukumu lake la kutoa elimu ya uongozi wa elimu.

Wakati huo huo amewaeleza wadau kuwa Serilali inakamilisha taratibu za uanzishwaji wa Bodi ya kitaaluma ya Walimu itayosimamia masuala yote ya taaluma hiyo.

 Akizungumzia nafasi ya wadau wa elimu amesisitiza kuwa Wizara inakaribisha maoni wakati wowote kwa kufuata taratibu za kiofisi.

Aidha amesema kupitia Kongamano wadau wametoa maoni ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika usimamizi na uboreshaji elimu ya ualimu katika Wizara.

Mwenyeki wa mkutano huo  Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi Rais -Tawala Mitaa na Tawala za Mikoa Tamisemi) George Jidamva ameishukuru Wizara ya Elimu kwa kuandaa mkutano huo na amesema kuwa TAMISEMI wakiwa waendeshaji wa shule pia watafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa mkutano.

Nae Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyuo Binafsi Mahmood Mringo amesema sekta ya elimu inazungumzwa na watu wasio wadau hivyo kila mdau atumie nafasi ya kuzungumza suala la elimu ili pamoja wadau wote tushiriki katika uboreshaji.

Amesema kuwa ukurasa mpya umefunguliwa na kuongeza nguvu katika kusukuma gurudumu la elimu mbele.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Evamaria Semakafu akizungumza wakati wa kufunga mkutano la wadau wa Elimu ya Ualimu kuhusu usimamizi na uendeshaji bora wa Elimu ya Ualimu uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Elimu ya Ualimu wakifuatilia hotuba Naibu Katibu   Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Evamaria Semakafu wakati akifunga mkutano wa wadau hao uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Ualimu Augusta Lupokela akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu ambapo amesema matokeo ya Mkutano huo yatasaidia katika maandalizi ya mpango mkakati wa maboresho ya usimamizi wa mafunzo ya ualim uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyuo Binafsi Mahmood Mringo akitoa neno la wa Mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu kuhusiana uwepo na ushirikishwaji wa sekta ya elimu kwa maendeleo ya Taifa uliofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu  Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Evamaria Semakafu akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano wa wadau wa elimu ya ualimu baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...