Naibu Waziri Tamisemi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Mwita Waitara amewakumbusha Wakurugenzi kutekeleza maelekezo ya kununua zana za kufundishia kwa watoto wa madarasa ya awali ili waweze kujifunza kwa vitendo na kukuza ubongo wao.

Waitara alisema kuwa, zana hizo ni muhimu na kwamba zinamsaidia mtoto kujifunza kwa njia rahisi na salama na kumuongezea uelewa katika elimu ya malezi na makuzi.

Alisema tayari serikali ilishatoa maelekezo kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua zana za kufundishi kwa wanafunzi wa madarasa ya awali, kwa sababu zina hizo zinasaidia kupanua uelewa wa watoto katika masuala ya elimu, malezi na makuzi.

"Tayari tumeshatoa maelekezo kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya elimu changamshi kwa madarasa ya awali ili waweze kupata elimu bora ya malezi na makuzi," alisema Waitara.

Anaongeza kuwa Mtoto anapotumia zana za kujifunzia kuanzia darasa la awali, anaelewa zaidi kuliko yule ambaye hajatumia kabisa, hivyo basi wakurugenzi wanapaswa kuhakikisha kuwa, zana hizo zinakuwepo ili watoto waweze kupata elimu bora.

Aliongeza kuwa,elimu bora inaanzia darasa la awali, kwa wanafunzi kuwa na vifaa vya kujifunzia hali ambayo imewafanya kutoa maelekezo hayo ili kuhakikisha wanaboresha utoaji wa elimu nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo,serikali utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa, elimu inayotolewa inakidhi viwango, hali ambayo itasaidia wanafunzi wanaomaliza kuingia kwenye soko la ushindani la ajira.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania wa mwaka 2016, ulibainisha baadhi ya zana zinazohitajika katika madarasa la awali ambazo ni pamoja na kibao fumbo, bao, karata, dadu, domino, chati ya mchezo wa ngazi na nyoka, drafti, vihesabio na midoli, kadi za herufi, kadi za namba, kadi za picha, vipande vya mbao, kanda za video, runinga, redio.

Baadhi ya picha za kutengeneza zinazofaa kufundishwa kwa watoto wa madarasa ya awali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...