NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WANAHISA zaidi ya 400 wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB) wamekutana mjini Mtwara katika mkutano wa mwaka (AGM) na kupokea taarifa ya kiutendaji ya benki hiyo kwa mwaka 2018.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw.Richard L. Makungwa amesema Mkutano huo wa tatu ni wa kawaida ambao lengo lake ni kuwapa taarifa ya kiutendaji ya benki ambapo wanahisa wataijadili na kuweka maazimio mbalimbali ya kiutekelezaji kwa wakati ujao.

“Sisi kama taasisi ya kifedha, kila mwaka huwa tunafanya mkutano wa wanahisa ili kuwaeleza hali ya benki yao, Shughuli zilizofanyika kwa mwaka mzima, mafanikio yaliyopatikana, changamoto na matarajio ya baadaye, lakini pia kupokea maoni kutoka kwa wanahisa wetu ambao pia ni wateja wetu wanayo nafasi kubwa sana ya kutoa maoni yao kwa nia ya kuboresha uendeshaji wa benki.” Alifafania Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Makungwa.
Alisema wengi wa Wanahisa wa Mwalimu Commercial Bank Plc ni walimu lakini pia wako wanahisa ambao sio walimu, kuna mashirika na taasisi nyingine kwani benki hii ipo kuhudumia Watanzania wote.
Mwalimu Commercial Bank Plc kama zilivyo benki nyingine za biashara inafanya shughuli zote za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa wateja wake.
“Benki yetu inatoa mikopo ya binafsi, mikopo ya biashara zikiwemo biashara ndogo ndogo na kwakweli tumekuwa na mafanikio makubwa, wateja wetu ni waaminifu wanarejesha mikopo waliyopewa pamoja na changamoto za hapa na pale lakini bado tunafanya vizuri katika eneo hilo.” Aibainisha.
Alisema licha ya benki kutumia mifumo yake ya kawaida katika kutoa huduma lakini pia inakusudia kuendeshwa kidigitali ili mteja popote alipo aweze kufanya miamala bila shida yoyote na hivi karibuni benki itajiunga na mtandao wa VISA ambao utawawezesha wateja wetu kupata huduma za kibenki mahala popote walipo.
“Benki inaendelea kuboresha huduma zake, wanahisa na wateja wetu  wategemee kuwa benki yao inaendelea kuboresha huduma zake na kuimarika walimu wetu ambao ndio wateja wetu wakubwa wako nchi nzima na tunajitahidi kuhakikisha huduma zetu zinawafikia kwa urasihi.” Alifafanua.
Alitoa hakikisho kuwa Mwalimu Commercial Bank Plc iko katika hali nzuri na mtaji wake uko vizuri na unakidhi matakwa ya msimamizi wa mabenki yaani BoT.” Alisema.
Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Herman Kessy alisema, benki imepata leseni ya uwakala wa bima na hivyo itawaomba wadau Chama cha Walimu (CWT), Mfuko wa Pensehni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutumia huduma hiyo kwa faida ya benki na wanahisa wote.
Pia Bw. Kessy alisema katika mafanikio ya benki kwa mwaka 2018 ni pamoja na kuongeza tawi la pili pale Mlimani city, lakini kufungua ofisi kwa ajili ya kutoa huduma kwenye mikoa ya Morogoro na Mwanza na Mbeya.
Awali wajumbe wa mkutano huo walipatiwa semina iliyoendeshwa na Meneja wa Huduma za kidijitali Bw. John Mhina iliyolenga kuwaelimisha nidhamu ya matumizi ya fedha na umuhimu wa kuweka akiba.
Wajumbe pia walipata elimu kuhusu soko la hisa umuhimu wa walimu kununua hati fungani ambapo Mkuu wa Uendeshaji na Fedha wa kampuni ya Core Security Limited ambayo ni wakala wa soko la hisa la Dar es Salaam,Bi. Mary Kessy alifafanua kuhusu namna ambavyo mtu anaweza kununua hati fungani.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Herman Kessy, (kuli), akizungumza wakati wa Mkutanio Mkuu wa tatu wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo kwenye ukumbi wa BoT mkoani Mtwara leo Agosti 22, 2019. Wengine kiutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Richard Makungwa, na Mjumbe wa Bodi Bw. Said Kambi.
 Bw. Kessy akihutubia wajumbe.
 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw.Richard L. Makungwa, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya Wanahisa wakifuatilia hotuba za viongozi.
 Wanahisa wakipitia taarifa mbalimbali kuhusu utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2018.
  Baadhi ya Wanahisa wakifuatilia hotuba za viongozi.
 Mwanahisa akipitia taarifa hiyo ya utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2018.
 Baadhi ya wajumbe wa bodi wakiwa pamoja na wanahisa wa benki hiyo wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi.
 Wajumbe wa bodi Profesa Tadeo Satta (kulia) na Bw.Framncis Ramadhani wakizungumza jambo.
 Mwanasheria wa benki akitoa ufafanuazi wa masuala mbalimbali yahusuyo mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Deus Seif (aliyesimama), akizunguzma kwenye mkutano huo.
 Wageni waalikwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania nao walikuwepo.
Afisa Mtendaji Mkuu  Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa (kulia), akizungumza jambo na Mkuu wa Rasilimali wa tu wa benki hiyo, Bi. Ellijalia  Mabiki.

Meneja wa Huduma za kidijitali Bw. John Mhina akitoa mada kuhusu umuhimu wa kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na kujenga tabia ya kujiwekea Akiba kwa kuweka pesa benki ya Mwalimu Commercial Bank Plc

Bw.Makungwa (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Fedha wa MCB, Bw. Selemani Kijori wakati wa mkutano huo.
Wajumbe wakipatiwa makabrasha yenye maelezo na ripoti ya mwaka ya benki hiyo.
Picha ya wajumbe wa Bodi na baadhi ya wanahisa wakubwa wa Mwalimu Commercual Bank Plc.
Picha ya pamoja wajumbe wa bodi na baadhi ya viongozi wa chama cha walimu CWT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...