Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas (kulia) akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mtafungwa baada ya kuwasili Mkoni Morogoro baada ya kutokea ajali ya lori lililoungua moto na kusababisha vifo vya watu 62 na wengine 72 kujeruhiwa katika eneo la Msamvu Itigi Mkoani humo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Maafa, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Nasser Mwakamboja.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas akikagua lori la mafuta lililopata ajali na kuungua moto Msamvu Itigi Mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu 62 na wengine 72 kujeruhiwa. Nyuma yake ni Mkuu wa Kitengo cha Maafa, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Nasser Mwakamboja
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akizungumza na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Maafa cha Jeshi la Polisi ACP Nasser Mwakamboja wakiwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro walipowasili kuona majeruhi walioungua moto baada ya kutokea ajali ya lori lililoungua moto na kusababisha vifo vya watu 62 na wengine 72 kujeruhiwa katika eneo la Msamvu Itigi Mkoani humo. Picha na Jeshi la Polisi.
========= ======== ========
*Wengine 70 wajeruhiwa, ni waliokuwa wanakuwanda kuzoa mafuta kwenye madumu
*Wengi wao ni vijana wa bodaboda...mashahidi waeleza iliyokuwa eneo la tukio
Na Said MwisheheMichuzi TV
INASIKITISHA
SANA! Ndivyo unavyoweza kuelezea kutokana na kufariki dunia kwa watu
62 na wengine 70 kujeruhiwa na moto huo baada ya kulipukiwa kwa moto
baada ya kukimbia kutoa mafuta ya petroli baada ya gari aina ya roli
kupinduka leo eneo la Msavu mkoani Morogoro.
Ajali
hiyo imetolewa leo Agosti 10,2019 asubuhi katika eneo hilo la Msavu
ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia.Michuzi TV kuwa roli ya mafuta
ilipinduka baada ya kumkwepa dereva bodaboda,hivyo roli likaacha njia.
Mmoja
wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Bathromeo amesema baada ya
ajali hiyo kutokea baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo walianza
kukimbia roli hilo wakiwa na madamu na ndoo wa ajili ya kubeba mafuta.
Hata
hivyo baada ya roli kupinduka yaliyoanza kumwagika yalikuwa mafuta ya
dizeli na nusu baadae yakaanza kutoka mafuta ya petroli."Ukweli mimi
tangu ajali inatokea nilikuwa hapa na nimeona kila kilichokuwa
kinaendelea.Wenzetu wenye tamaa waliamua kwenda na madamu yao kuchukua
mafuta,tuliwakataza lakini kwa tamaa zao waliamua kwenda.
"Hapa
kuna mama alikuwa anauza chakula lakini baada ajali kutokea akachukua
ndoo zake na kwenda kujaza mafuta na kisha kuyaweka hapa kwenye eneo
analopikia.Matokeo yake yeye na mtoto wake wamekufa.Inasikitisha sana
lakini ajali za aina hii zimekuwa zikitokea ila wananchi
hatujifunzi,"amesema shuhuda huyo.
Kwa
upande wake shuhuda mwingine amesema vijana waliokuwa eneo hilo
yakiwemo wateja na waendesha bodaboda walionekana kubeba madamu na
kwenda kuchota mafuta lakini ghafla ukasikika mlipuko mkubwa ambao
tulisababisha gari hiyo kuanza kuwaka moto ambao ulikuwa unasambaa kwa
kasi kubwa.
Hivyo
kutokana na moto huo waliokuwa wakizoa mafuta wakaanza kuungua na wengi
wamekuwa kwa kuteketea kwa moto huo ."Wamekufa watu wengi sana kwenye
ajali hii ya kulipuka kwa roli la mafuta eneo hili la Msavu.
Amesema
kuna baadhi yao walijaribu kukimbia lakini wakati huo tayari moto
ulishakuwa umesambaa mwilini na kwamba kuna mmoja alijaribu kupanda juu
ya moto lakini mti nao kuanza kuweka.
Hata
hivyo tayari viongozi wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Morogoro
wamezungumzia ajali hiyo ambayo imesababisha vifo vya watu hao na kwamba
wataendelea kutoa taarifa zaidi ya idadi ya rasmi ya waliopoteza maisha
na waliojeruhiwa ingawa tayari watu 62 wameriporiwa kupoteza maisha na
wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa kwa moto.
Wakati
huo huo Kamanda mstaafu wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaaam
Suleiman Kova ambaye kwa sasa Mkurugenzi wa taasisi binafsi
iliyosimamia maafa na majanga amesema ajali hiyo inasikitisha kwani
idadi kubwa ya nguvu kazi imepotea.
Kova
amesema kwa taarifa zilizopo hadi mchana huu tayari wameporipotiwa watu
62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 70 wameungua na moto huo na
sasa wakimbikizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuokoa maisha yao.
"Ni
ajali mbaya sana,watu wengi wamepoteza maisha.Ukweli wengi waliopoteza
maisha ni wale waliokuwa wanakwenda kuchukua mafuta baada ya roli
kupinduka. Ni mara nyingi elimu imekuwa ikitolewa kuhamasisha wananchi
kutokimbilia mafuta baada ya gari kupinduka.
"
Ni mara nyingi tumeshuhudia matukio ya aina hii na watu wamekuwa
wakipoteza maisha.Ndio maana enzi zetu tuliamua kuanzisha Polisi
shirikishi ili wananchi wenyewe kwa wenyewe wazuiane, Hata hivyo moto ni
jambo la dharura,hivyo hakuna wa kulaumiwa na hata waliokufa hatuwezi
kuwalaumu," amesema Kova.
Ametoa
rai kwa wananchi kujiepusha na majanga kwa kuhakikisha wanachukua
tahadhari na kusisitiza ajali hiyo ni mafunzo huku akitumia nafasi hiyo
kutoa pole kwa Rais,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Watanzania wote kwani
msiba huo ni mkubwa.
Pia
viongozi wa dini wamezungumzia ajali hiyo ambapo kwa sehemu kubwa
wamesisitiza jamii.kujenga utamaduni wa kuchukua tahadhari na kubwa
zaidi ni ajali inatopotokea cha kwanza ni kusaidia waliopata ajali
badala ya kufanya tofauti na hivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...