Wenyeji Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi tayari kwa kushiriki mashindano ya FEASSSA 2019 Jijini Arusha.
Wenyeji Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi tayari kwa kushiriki mashindajo ya FEASSSA 2019 Jijini Arusha.
Washiriki kutoka nchini Kenya wakiwa tayari kushiriki mashindano ya FEASSA Jijini Arusha.
Washiriki kutoka Zanzibar wakipita mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya RIs TAMISEMI,Mhe.Suleiman JaffoWashiriki kutoka Uganda wakipita mbele ya mgeni rasmi waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe.Suleiman JaffoWashiriki kutoka nchini Rwanda wakipita mbele ya mgeni rasmi Waziri wa nchi TAMISEMI ,Mhe.Suleiman JaffoNgoma ya wanafunzi kutoka mkoani Geita ikiwa inatumbuiza wakati wa ufunguzi wa mashindani hayo rasmi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akizungumza na wachezaji kabla ya kuanza kwa mechi ya uzinduzi kati ya timu mojawapo kitoka nchini Kenya na Tanzania katika uwanja wa Kumbukumbu ya Shekh Amri Abeid Karume Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akikagua timu pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kabla kuanza kwa mechi ya uzinduzi kati ya timu mojawapo kitoka nchini Kenya na Tanzania katika uwanja wa Kumbukumbu ya Shekh Amri Abeid Karume Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akikagua wachezaji mechi uzinduzi kati ya timu mojawapo kutoka nchini Kenya katika uwanja wa Kumbukumbu ya Shekh Amri Abeid Karume Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akisalimiana na wachezaji kabla ya kuanza kwa mechi ya uzinduzi kati ya timu mojawapo kutoka nchini Tanzania katika uwanja wa Kumbukumbu ya Shekh Amri Abeid Karume Jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mashindano ya Shirikisho la michezo linaloundwa na nchi Wananchama wa Jumuiya za nchi za Afrika ya Mashariki limezinduliwa rasmi hapo jana mkoani Arusha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo katika uwanja wa kumbukumbu ya Shekh Amri hAbeid na kuhuduriwa na wanafunzi kutoka nchi mbalimbali wapatao 3500 

Akizungumza katika uzinduzi wa shirikisho hilo Waziri Jaffo amesema michezo hiyo iwe ni fursa kwa vijana wa Jumuiya hiyo kuibua vipawa mbalimbali vya kitaifa na kimataifa ,huku akiwataka viongozi wanchi wananchama kulea vipawa vilivyoko ndani ya vijana hao ili ije kuwa tunu katika mataifa ya Afrika ya Mashariki.

Jaffo amesema kuwa watumie jukwaa hilo la michezo kama fursa ya kujenga uzalendo,kwa kupiga vita madawa ya kulevya,maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na wizi ,ujambazi sambamba na vitendo ambavyo siyo vya kiuugwana,pia michezo hiyo watakwenda kuibua vipawa mbalimbali vya Kimataifa 

Aidha amesisitiza Kuimarisha upendo miongoni mwa vijana sambamba na kuushukuru uongozi mzima wa FEASSSA 2019 kwa kuipa heshima nchi ya Tanzania heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo katika mkoa wa Arusha ambalo ni Jiji la kitalii kwani wageni hao watapata pia fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu katibu mkuu anayeshughulikia Elimu Tamisemi Txson Nzunda amesema malengo makubwa ya michezo michezo hiyo inamanufaa makubwa kwa Wanaafrika ya Mashariki na wanachama wa Feassa kwa ujumla katika kujenga kukuza na kuendeleza michezo,kujenga wigo miongoni mwa wananchama wa EAC na nchi majirani pamoja na mashirika mengine ya kitaifa na kimataifa yanayojihusisha na michezo ndani na nje ya jumuiya hiyo.

Amesema kuwa FEASSSA pia inawajengea motisha kwa wakuu wa shule ambao wanasaidia kuimarisha taaluma ya michezo kama sehemu ya kutekeleza majukumu yao ya kuwajenga watoto katika na kuhakikiha kwamba Elimu bora inatolewa itakayowawezesha kushindana Kikanda na Kimataifa ili vijana wawe mfano katika Nyanja za Kimataifa.

Amesisitiza kuwa kupitia michezo hiyo wanajenga umoja miongoni mwa watoto wa jumuiya hiyo hivyo malengo yake haswa ni kukuza fani za michezo kwa wanafunzi kwa kuwashindanisha ili kubaini na kukuza vipaji vya wana wa Afrika ya mashariki,kuendeleza na kudumisha mshikamamno,upendo miongoni mwa wanafunzi,waalimu na viongozi wan a wanachama wa feassa kwa ujumla wake.

Amesema wanaratibu mafunzo semina ,warsha na maelekezo mengine ya viwango vya vya michezo vya Kitaifa na vya Kimataifa miongoni mwa wanachama ili kuwajengea uwezo wa kuweza kufanya vizuri kwa kuamini kwamba kwa kupita miachezo FEASSSA watatoa timu bora na kuleta mapinduzi ya michezo ndani ya jumuiya ya Afrika ya mashariki sambamba na kuhamasisha elimu ya kujitegemea mashuleni na kujenga uimara wa kujitegemea miongoni mwa watoto

Txson Nzunda amesema wanafunzi 3500 Idadi ya wanafunzi wa sekondari ni 2800,wanafunzi wa shule za msingi ni 700 pia viongozi wa michezo na waratibu kwa maana ya waamuzi ,makocha wauguzi,waalimu pamoja na viongozi waelimu wapatao 770.Shirikisho hilo limewalenga wanafunzi wa sekondari wanchi wananchama kwa kila nchi husika ikiwemo Burundi,

Tanzania, Kenya,Uganda,Rwanda,na sudani kusini,mashindano hayo yaliwahi kufanyika mwaka juzi( 2017)Jijini Dar es salaa ambapo huu mwaka 2019 FEASSSA imewamewakaribisha Nchi ya Malawi.

Aidha mashindano hayo yatadumu kwa muda wa siku kumi ndipo yatamalizika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...