Na Jusline Marco, Arusha

Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi ameagiza wezi wa mboga mboga katika bustani za mradi unaofadhiliwa na TASAF katika shule ya msingi ya Elerai wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwani wamehujumu fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kaya masikini ziweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea miradi inayotekelezwa na serikali ikiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Elerai,Afisa huyo ameshangazwa na kitendo hicho ambacho kinawakatisha tamaa kinamama wanaolima bustani hizo pamoja na wawezeshaji wa mradi huo.

Cholobi amesema kuwa mradi huo hauna haja ya kuwekewa mlinzi maalumu kwani utaongeza gharama za utekelezaji hivyo polisi jamii wanapaswa kuulinda mradi kwa kushirikiana na wananchi kwani fedha hizo niza serikali pamoja na wadau wa maendeleo.

Vilevile ameuagiza uongozi wa kata kukutana na kujadili juu ya namna ya kuwashirikisha wadau wa maendeleo katika kumalizia miradi ambayo bado haijakamilika ili iweze kukamilika ikiwemo ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule hiyo ya msingi.

Naye Mtendaji wa kata ya Lemara Johari Kitara amesema kuwa mradi huo ulianzishwa na Tassaf kwa lengo la kuwakomboa kinamama ili wapate kipato na kujiendeleza hivyo changamoto hiyo itashughulikiwa.
Afisa tarafa Erelai Mkoani Arusha akitoa maelekezo kwa askari polisi kuhusu ulinzi wa bustani hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...